Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Nchi za Kiislamu zinapaswa kuimarisha umoja wa Waislamu na kutetea haki zao
2010/03/04 - 16:03
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei leo amekutana na viongozi wa serikali na wananchi wa matabaka mbalimbali kwa mnasaba wa kuadhimisha Maulidi ya Mtume wa nuru, uadilifu na rehma Muhammad (saw) na mjukuu wake Imam Ja'far Swadiq (as). Ayatullah Khamenei amesisitiza katika hadhara hiyo kwamba kuzalisha upya hakika na maarifa ya Kiislamu na kutekeleza mafundisho ya Mtume wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu ndiyo haja kubwa zaidi ya umma wa Kiislamu. Amesema kuwa umoja na mshikamano wa wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu ndio wenzo wa kutatua matatizo mbalimbali na sababu ya maendeleo na ustawi wa ulimwengu wa Kiislamu.