Ayatullah Khamenei asema katika hotuba za Swala ya Ijumaa:
Iran italisaidia taifa lolote litakalosimama kupambana na utawala ghasibu wa Israel
2012/02/03 - 18:21
Sambamba na siku hizi za kuadhimisha mwaka wa 33 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khameni leo amehutubia Swala ya Ijumaa mjini Tehran akitoa uchambuzi kamili kuhusu matunda na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuzungumzia masuala muhimu ya ndani, vitisho vya maadui na hali ya kieneo na kimataifa na vilevile uchaguzi ujao wa Bunge la 9 la Iran.