Maafisa wa msafara wa Hija wa Iran wakutana na Kiongozi Muadhamu
Maafisa wa msafara wa Hija wa Iran wakutana na Kiongozi Muadhamu
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu akihutubia maafisa wa Hija:

Usalama, izza na huduma bora kwa mahujaji vinapaswa kudhaminiwa

Kongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia hadhara ya maafisa wa msafara wa Hija wa Iran waliokwenda kuonana naye na kusema kuwa, ibada ya Hija ni chombo kisichokuwa na kifani cha kiroho na kijamii na eneo bora zaidi kwa ajili ya kueleza itikadi na misimamo ya Umma wa Kiislamu. Amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitasahau maafa ya Hija y...
Idara ya Mahakama inabeba bendera ya kutetea haki na uhuru
Idara ya Mahakama inabeba bendera ya kutetea haki na uhuru
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amekutana na kuhutubia hadhara ya maafisa wa Idara ya Vyombo vya Mahakama na wakuu wa mahakama zote hapa nchini. Ameashiria uwezo na nafasi ya juu na makhsusi ya Idara ya Mahakama na taathira zake katika usimamizi wa nchi na kusema, kuna udharura wa kuwepo mtazamo wa kimageuzi katika idara hiyo. Ameongeza kuwa: Idara ya Mahakama inapaswa k...
Kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kupambana na mfumo wa ubeberu
Kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kupambana na mfumo wa ubeberu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alasiri ya jana alizungumza na mamia ya wahadhri wa vyuo vikuu, wanachama wa jumbe za kielimu, watafiti na wasomi wa vyuo vikuu katika kikao kilichoendelea kwa kipindi cha zaidi ya masaa mawili. Katika Kikao hicho Ayatullah Khamenei ameeleza mchango usio na mbadala wa wahadhiri wa vyuo vikuu katika kulea wanafunzi na kutengeneza mafasi ya Iran katika...

Anwani nyingine

Zidisheni uwezo wa jeshi ili madhalimu watishike
Husainia ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) mjini Tehran leo (Jumatano) ilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Ali Khamenei ambaye ni Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran ametembelea maonyesho hayo kwa muda wa zaidi ya masaa mawili na kuona kwa karibu teknolojia za kisasa na za ndani ya Iran za taasisi za elimu za kimsingi ambayo ni matunda ya jitihada, ubunifu, maarifa na utafiti wa wataalamu wa ndani ya nchi na ambayo yana taathira ya moja kwa moja katika kuzidisha uwezo wa kijeshi wa vikosi vya ulinzi vya Iran.
Kiongozi Muadhamu azuru Haram ya Imam Khomeini
Zikiwa zimekaribia siku za Mwenyezi Mungu za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanayoanza siku aliporejea kishujaa nchini Iran, Imam Khomeini (MA), Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi amekwenda kufanya ziara katika Haram ya mwanachuoni huyo mkubwa, na sambamba na kumsomea al Fatiha, amemuenzi na kumuombea dua mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kuna udharura wa kupanuliwa zaidi anga ya usomaji vitabu hapa nchini
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo Jumapili ametembelea Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran kwa kipindi cha masaa mawili.
Katika shughuli hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, wasimamizi wa vyumba mbalimbali vya maonyesho hayo walitoa maelezo kwa Kiongozi Muadhamu kuhusu vitabu vyao na shughuli za uchapishaji vitabu.