Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu apanda mche wa mti katika Wiki ya Maliasili

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei leo mchana (Jumatano) amepanda mche mmoja wa mti katika Wiki ya Maliasili na Siku ya Kupanda Miti nchini Iran.

Baada ya kupanda mche huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amezungumza machache akiwashukuru wale wote wanajishughulisha na kazi ya kueneza maeneo kijani nchini Iran na kuongeza kuwa: Wakuu na matabaka yote ya wananchi wa Iran wanataka suala la maeneo kijani lipewe umuhimu mkubwa ili nchi na maisha ya wananchi yaweze kufaidika na neema hiyo kubwa ya Mwenyezi Mungu.

Amesema, suala la kulinda mazingira ni muhimu sana na huku akiashiria matukio kama ya kuingia hewa ya vumbi na mchanga nchini Iran kutoka nchi jirani amesisitiza kuwa: Ili kuondoa madhara hayo, sekta zote za serikali zinapaswa kulipa umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na madhara hayo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa, kuzungumza na nchi husika na kushirikiana na pande mbalimbali kwa ajili ya kuzuia madhara hayo.

Ayatullah Ali Khamenei vilevile ametaka suala la kuzuia kuharibiwa mazingira na maeneo kijani lipewe umuhimu mkubwa zaidi akisema: Kaulimbiu ya "Kila Muirani, Mti Mmoja" ni nara na kaulimbiu nzuri sana na ni ya dharura kwa ajili ya kupambana na kugeuzwa vyanzo hivyo muhimu vya kimaumbile kuwa vyuma na saruji kama ambavyo pia jambo hilo ni la dharura kuwa nalo maafisa wote husika kama wenzo wa kupambana kisheria na watu wote wanaotumia vibaya jambo hilo.

Zoezi hilo limehudhuriwa na Waziri wa Jihadi ya Kilimo, Mwakilishi wa Fakihi Mtawala katika Wizara ya Jihadi ya Kilimo na meya wa jiji la Tehran.

 

700 /