Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Viongozi wa kidini, kisiasa, wasanii na wanamichezo wamjulia hali Kiongozi Muadhamu

Kiongozi Muadhamu anaendelea kupata matibabu hospitalini hapo baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi kibofu siku chache zilizopita.

Ayatullah Amini alimtembea Kiongozi Muadhamu alasiri ya leo na kumwombea dua kwa Mwenyezi Mungu ampe shifaa na afya kamili.

Vilevile mawaziri kadhaa wa serikali, Makamu wa Rais, wawakilishi wa Faqihi Mtawala mikoani na katika taasisi mbalimbali za kimapinduzi, wawakilishi wa Ayatullah Safi Golpayegani, Makarim Shirazi, Musavi Ardebili, Kabuli na Sayyid Hakim, baadhi ya wanachama wa Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu na Baraza la Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu na kadhalika wamemtembelea na kumjulia hali Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Vilevile jana na leo baadhi ya wasanii, wadau wa masuala ya utamaduni na fasihi, wanahabari na wanamichezo wamefika hospitalini hapo na kumjulia hali Ayatullah Ali Khamenei.    

               

700 /