Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Al Maliki amefanya juhudi za kuzua mivutano Iraq

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amemkaribisha ofisi kwake na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Iraq Nouri al Maliki aliyeko safarini hapa mjini Tehran. Katika mazungumzo hayo Ayatullah Ali Khamenei amepongeza ushujaa, uwezo na uongozi bora wa al Maliki wakati alipokuwa Waziri Mkuu wa Iraq na huduma kubwa alizotoa katika kulinda utulivu, kujitawala na maendeleo ya nchi hiyo.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amemwambia Nouri al Maliki kwamba: “Wakati wa kukabidhi madaraka ya nchi umefanya kazi kubwa kwa ajili ya kuzuia machafuko na mivutano nchini Iraq na hatua hiyo kamwe haitasahaulika nchini Iraq”.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia jinsi al Maliki anavyoelewa vyema matatizo na masuala mbalimbali ya Iraq na akasema: “Mwenendo wako wa kuisaidia serikali mpya ya Bwana Haidar al Abadi na vilevile juhudi za kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa makundi mbalimbali ya Iraq ni hatua nzuri ambayo inapaswa kudumishwa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Iraq Nouri al Maliki ameeleza kufurahishwa kwake na mazungumzo yake na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akasema kuwa Jamhuri wa Kiisalmu ya Iran daima imekuwa mstari wa mbele kutoa msaada mkubwa zaidi kwa serikali na wananchi wa Iraq kwa ajili ya kukabiliana na magaidi na vibaraka wa kigeni.      

 

700 /