Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Iran itaendelea kusimama imara hadi Palestina itakapokombolewa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kadhia ya Palestina ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete hadi pale malengo ya Palestina yatakapotimia na hapana shaka kuwa vijana watashuhudia siku hiyo.

Ayatullahil Udhmaa Ali Khamenei ameyasema hayo leo katika mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina, Ahmad Jibril. Amepongeza huduma na juhudi kubwa za Katibu Mkuu wa harakati hiyo katika njia ya kupigania malengo ya Wapalestina na akasema: Ahmad Jibril ni miongoni mwa nguzo muhimu za kadhia ya Palestina.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza matarajia kwamba mapambano ya Palestina yataendelea hadi utakapopatikana ushindi wa mwisho.

Kwa upande wake Ahmad Jibril ameeleza kufurahishwa kwake na kukutana na Kiongozi Muadhamu na kusema Mapinduzi ya Kiislamu yameifanya Iran kuwa nchi yenye taathira kubwa katika uwanja wa kimataifa na kwamba maendeleo ya sasa ya Iran yamepatikana chini ya usimamizi wa busara na hekima wa Walii wa Waislamu duniani Ayatullah Ali Khamenei. Ahmad Jibril pia amepongeza misimamo imara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kutetea haki za taifa la Palestina
700 /