Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Khamenei:

Changanyeni elimu, kutafakari na ucha Mungu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma risala kwa kikao kikuu cha arubaini na tisa cha Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu barani Ulaya na akiwanasihi vijana kwa kusema, ambatanisheni kazi ya kutafuta elimu na kutafakari, na yote hayo mawili yachanganyeni na ucha Mungu na kutakasa nafsi; wakati huo hakuna hazina itakayolingana na kuwa sawa na hiyo kwa nchi yenye utajiri wa vijana kama nyingi.

Ujumbe huo umesomwa katika Msikiti wa Kabud (Blue Mosque) huko Yerevan, mji mkuu wa Armenia na Hujjatul Islam Walmuslimin Javad Ejei, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya wanachuo wa barani Ulaya. Matini kamili ya ujumbe huo ni hii ifuatayo:

 Bismillahir Rahmanir Rahim

Vijana! Wapendwa!

Kuwepo kwenu kwenye vituo vya vyuo vikuu vya nchi mbalimbali ni fursa nzuri sana ya kukuwezesheni kuwa na muono mpana uliojaa hekima na maarifa kuhusiana na matukio mbalimbali yanayojiri duniani. Jambo hilo pia linaipa Iran ya baadaye fursa ya kuwa na wasomi wanaoijua vyema dunia na weledi. Mnapaswa kuthamini sana fursa hiyo.

Kupotoka kuna madhara makubwa kwa kiwango kile kile cha mghafala. Leo hii mnapaswa kulipa umuhimu wa aina yake na wa kipekee swali kwamba, kwa nini siasa za Magharibi zinalishikilia na kuling'ang'ania suala la kueneza chuki na woga kuhusu Uislamu? Mnapaswa kulipa umuhimu mkubwa suala la kuangalia na kuona ni kitu gani chenye nguvu katika Uislamu wa kisiasa kwa mtazamo wa Iran ambacho madola ya kibeberu yenye chuki, vamizi na yanayopenda kutawala mataifa mengine, yanakabiliana nacho kwa nguvu zao zote?

Ambatanisheni kazi ya kutafuta elimu na kutafakari, na yote hayo mawili yachanganyeni na ucha Mungu na kutakasa nafsi; wakati huo hakuna hazina itakayolingana na kuwa sawa na hiyo kwa nchi yenye utajiri wa vijana kama nyingi.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu akusaidieni na akupeni taufiki katika juhudi zenu.

Sayyid Ali Khamenei,

3/11/1393 (Hijria Shamsia)

Januari 23, 2015

700 /