Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Siku chache kabla ya kuanza Alfajiri 10:

Kiongozi Muadhamu azuru Haram ya Imam Khomeini

Zikiwa zimekaribia siku za Mwenyezi Mungu za Alfajiri Kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanayoanza siku aliporejea kishujaa nchini Iran, Imam Khomeini (MA), Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi amekwenda kufanya ziara katika Haram ya mwanachuoni huyo mkubwa, na sambamba na kumsomea al Fatiha, amemuenzi na kumuombea dua mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu.

Vilevile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefanya ziara kwenye makaburi ya mashahidi wa Tir 7 -kwa mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia- na kwenye makaburi ya mashahidi wengine ya Behesht Zahra -kusini mwa Tehran-, na kuwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu awapandishe daraja za juu peponi.

 

700 /