Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aipongeza timu ya mieleka ya Iran kwa kushinda kombe la dunia

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe akiwapongeza wanamieleka wa Iran baada ya timu ya taifa ya mieleka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuibuka na ushindi katika mashindani ya dunia ya mchezo huo uliofanyika jana nchini Marekani.

Matini kamili ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ni hii ifuatayo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Ninawapongeza wanamieleka na maafisa wote wa timu ya taifa ya mieleka kwa kupata ushindi katika mashindano ya kombe wa dunia ya mieleka, na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuona wanangu wakiweza kwa mara nyingine kulifaharisha taifa la Iran katika medani ya kimataifa.

Sayyid Ali Khamenei

24/ farvardin 1394

13 Aprili 2015 

700 /