Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Kuna udharura wa kuzalisha bidhaa za Kiislamu zenye mvuto

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, leo (Jumatatu) ameonana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na wajumbe wa Baraza Kuu la Masuala ya Intaneti la Iran na kulitaja baraza hilo kuwa ndicho kituo kikuu cha kuweka sera kwa uangalifu mkubwa, kwa kuzingatia majukumu na kwa kujiamini kuhusiana na masuala ya intaneti. Ameashiri kuzidi kukua na kupanuka kwa kasi kubwa suala hili la kipekee la Intaneti amesisitiza kuwa: kuna ulazima wa kutumia uwezo na vipaji vya vijana nchini Iran na kwa kubuni sera sahihi na hatua makini na zenye uratibu mzuri wa pamoja tena bila ya kupoteza muda, kupigwe hatua za haraka na za maana za kutoka katika hali ya kusubiri kutoa radiamali katika uga wa Intaneti na kuingia kwa nguvu zote kwenye medani hiyo kwa lengo la kuwa na taathira kubwa, nzuri na kuzalisha masiala ya Kiislamu yenye umakini na mvuto mkubwa.
Vilevile ameashiria tathira kubwa ya Intaneti ikiwa ni nguvu ya kipekee katika nyuga tofauti zikiwemo za utamaduni, siasa, uchumi, mtindo wa maisha, imani, itikadi za kidini pamoja na maadili na amesisitizia ulazima wa kuweko mipango madhubuti na makini ya kuweza kulinda mipaka ya usalama wa kifikra na kimaadili wa jamii katika uga huo. Ameongeza kwamba: Sharti la kuweza kuwa na taathira kubwa katika masuala ya Intaneti ni kuwawa makini katika kuchukua maamuzi, azma kubwa katika utekeleza bila ya kuporeza wakati, uratibu kati ya taasisi mbalimbali na kujiepusha na mambo yanayokwenda pamoja na kupingana.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vilevile amelitaja suala la kuwa na mipangilio mizuri na uungaji mkono wa Serikali hususan kitengo cha elimu na teknolojia cha Ofisi ya Rais kwa ajili ya kupanua sekta inayohusiana na teknolojia ya mawasiliano, kuwa ni jambo la dharura sana.
Amesisitiza kuwa: Kupanulia wigo wa sekta hiyo kupitia mashirika ya elimu msingi kutakuwa na taathira kubwa nzuri katika kuandaa nafasi za kazi na kuleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
Ayatullah Khamenei vilevile amemshukuru mheshimiwa Rais na wajumbe waliopita wa Baraza Kuu la Masuala la Intaneti la Iran pamoja na makatibu wa hivi sasa na wa zamani wa baraza hilo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Muhandisi Entezari, Katibu wa Baraza Kuu la Masuala ya Intaneti la Iran wametoa ripoti fupi kuhusu umuhimu wa Intaneti na udharura wa kuwa na ratiba na mipangilio mizuri kwa ajili ya kuingia kikamilifu katika uga huo. Vilevile wameelezea hatua zilizochukuliwa na baraza hilo na Kituo cha Taifa cha Intaneti katika kipindi cha kwanza cha utekelezaji wa majukumu yake.
Vilevile Ayatullah Amoli Larijani, Mkuu wa Chombo cha Mahakama nchini Iran amezungumzia nukta kadhaa muhimu kuhusu mambo ya lazima katika masuala uwanja wa Intaneti nchini.
700 /