Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Lengo la adui ni kudhoofisha itikadi za kidini na kisiasa na kuwahadaa vijana

Hotuba iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hadhara ya wajumbe wa Kamati ya Kongamano la Mashahidi wa Mkoa wa Chaharmahal na Bakhtiari hapo tarehe 13/07/1394 (05/10/15) imetolewa leo asubuhi katika eneo la ibada ya Swala la Imam Khomeini huko Shahrekord.
Katika hadhara hiyo Ayatullah Ali Khamenei aliashiria njama na hujuma za kila upande za kitamaduni, kiitikadi na kisiasa za adui kwa kutumia nyenzo mbalimbali dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kwamba, miongoni mwa malengo ya mipango ya jeshi la kisiasa na kiutamaduni la adui ni kudhoofisha itikadi za kidini na kisiasa na kufanya juhudi za kuwateka wanaharakati vijana na wenye taathira katika nyanja mbalimbali.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza juhudi na harakati zinazofanywa sasa na mrengo wenye imani, Hizbullah na maafisa wanaowajibika dhidi ya hujuma hiyo ya adui na kusema: Kazi zinazohusiana na kueneza na kuimarisha zaidi maana na mambo muhimu kama jihadi, shahada na kuuawa shahidi na kuwa na subira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa kazi muhimu zinazoweza kuzima na kubatilisha njama za adui.
Amesema sharti la kufanyika kazi hiyo ya kueneza maana hizo za kimsingi ni kuwakinaisha na kuwaridhisha wakusudiwa na kutumia nyenzo za sanaa na ulinganiaji. Ameongeza kuwa wanafikra na wasanii wanapaswa kushirikiana kwa lengo la kuzalisha bidhaa zenye taathira, na jambo hilo ni wadhifa wa maafisa wa serikali na wasio wa serikali na vilevile makundi ya wananchi wenye imani.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameashiria ari, ikhlasi na mahudhurio makubwa ya wananchi wa mkoa wa Chaharmahal na Bakhtiari katika nyanja mbalimbali za Mapinduzi ya Kiislamu na kujihami kutakatifu na akasifu ushujaa wa watu wa mkoa huo.           

700 /