Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Lengo la Marekani ni kutokomeza mapambano ya taifa la Venezuela

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mpainduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumatatu) ameonana na kuzungumza na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ambapo amesifu mapambano na harakati ya kuvutia ya Venezuela katika kukabiliana na siasa za uistikbari na kusisitiza: Leo siasa siasa za uistikbari ni kama balaa kubwa lililoikumba jamii ya mwanadamu na njia pekee ya maendeleo na ushindi kwa nchi huru zinazojitawala ni kupambana na kuwategemea wananchi katika vita vya matakwa.
Huku akiashiria siasa za tamaa za Marekani katika eneo la Latin Amerika Ayatullah Khamenei ameongeza: Marekani alikuwa ikilichukulia eneo hilo kuwa eneo lake la faragha lakini harakati ya aina yake ya Venezuela imeweza kulibadilisha eneo hilo kuwa eneo huru na lenye utambulisho maalumu. Kiongozi Muadhamu amesema lengo la Marekani ni kuyatokomeza mapambano ya kuvutia ya serikali na taifa la Venezuel na kuongeza: Vita vya leo duniani kwa hakika ni vita vya matakwa na nyinyi kwa kusimama imara na kuimarisha matakwa pamoja na kunufaika na uwezo mkubwa wa nchi yenu mtaweza kuyashinda matatizo. Ayatullah Khamenei ameashiria mfano bora wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kuupindua utawala tegemezi na uliojizatiti kwa silaha wa Pahlawi na kusema: Imam Khomeini (MA) huku akiwa mkono mtupu lakini kwa kutegemea nguvu ya wananchi na kuwaleta uwanjani aliweza kuingusha serikali iliyokuwa ikungwa mkono na Marekani pamoja na Ulaya, na njia ya ushindi na kudumishwa kwa mafanikio haya kwa serikali nyinginezo huru ni kutumia mbinu hiihii. Amesema maendeleo makubwa ya kielimu na teknolojia ya kushangaza ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na kuwepo kwa mashinikizo makubwa na vikwazo vya maadui ni uzoefu wenye thamani kubwa na kuongeza: Uzoefu huu ulitokana na kutegemea na kushirikiana na wananchi, na ufunguo wa kutatuliwa matatizo ni kuvutia hisia na nyoyo za wananchi kwa kuwafanyia kazi na kuwahudumia kwa moyo mkunjufu. Ayatullah Khamenei vilevile amesisitiza juu ya kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Iran na Venezuela na kusema: Iran inayachukulia maendeleo na mafanikio ya Venezuela kuwa ni maendeleo na mafanikio yake pia.
Katika mazungumzo hayo ambapo pia Bwana Jahangir, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alihudhuria, Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameelezea kuridhishwa kwake na kukutana tena na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa Iran ni nchi ambayo ina utambulisho wa kihistoria na kuwa nchi mbili za Iran na Venezuela ni marafiki halisi ambao wana uhusiano imara. Rais Maduro ameashiria heshima na hamu kubwa aliyokuwanayo marehemu  Hugo Chaves rais wa zamani wa Venezuela na Iran pamoja na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza: Mimi pia nimejifunza mambo mengi kwa kukutana na wewe na matamshi na ushauri wako umekuwa na athari nyingi kwangu. Rais wa Venezuela amesisitiza udharura wa kusimama imara na kulinda kujitawala kwa taifa na kusema: Ubeberu kwa kuchochea mvurugiko na hali ya mchafukoge duniani na kudharau utambulisho wa mataifa, una lengo la kutokomeza kujitawala kwa mataifa. Huku akiashiria utayarifu wa serikali na taifa la Venezuela kwa lengo la kukabiliana na njama za Marekani, Rais Maduro amesema: Kama ulivyosisitiza tunapasa kutumia vita vya matakwa na kwa kuwategemea wananchi ili kuwashinda maadui. Rais wa Venezuela amekumbusha umuhimu wa kikao cha nchi zinazouza nje gesi kwa wingi na kuhuishwa nafasi ya Opec na kuongeza: Tunapasa kubuni mipango mipya ya kunyanyua kiwango cha ushirikiano wa pande mbili na utekelezwaji wa miradi ya pamoja na kulinda pamoja na kuimarisha uhusiano wetu kama ilivyokuwa huko nyuma.

700 /