Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Jumuiya za Kiislamu za Wanachuo wa Barani Ulaya:

Azma kubwa ya vijana na wanachuo ndiyo njia pekee ya kubatilisha njama za adui

Matini ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu iliyosomwa jana Ijumaa na Hujjatul Islam Walmuslimin Javad Ejei, mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika masuala ya wanachuo wa barani Ulaya kwenye kikao cha 50 cha kila mwaka cha umoja huo kilichofanyika mjini Milan, Italia ni hii ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim

Kwa vijana wapendwa
Hivi sasa umoja wenu umetimiza miaka khamsini na umoja huo ni chombo kilichobarikiwa ambacho kimeunganisha pamoja uongofu wa Kiislamu na shauku na unyofu wa imani na kujipamba kwa sifa za ujana na uanachuo na matunda yake yanaweza kuwa ni kuzaa watu wasomi, wenye hekima, wanaomcha Mwenyezi Mungu na wenye muono wa mbali.
Fanyeni jitihada za kuhakikisha kuwa mnajioanisha kadiri mnavyoweza - nyinyi na umoja wenu - na malengo hayo makubwa na yenye kuleta ufanisi.
Nchi na taifa lenu linakuhitajieni watu kama nyinyi katika jitihada zake za kuvuka njia hii ndefu. Nia ya kweli na jitihada zenu zisizosita na za vijana na wanachuo wote wa Iran ni muhimu mno katika juhudi za kuzifelisha na kuzifanya tasa njama zote za kambi ya adui iliyosimama kukakabiliana na Iran ya Kiislamu iliyojaa fakhari, kambi ambayo inatumia silaha za kila namna kuendeshea njama zake hizo. Nyoyo zenu zilizojaa matumaini na uwezo wenu uliojaa nguvu za kimaada na kimaanawi ziwekeni tayari tayari wakati wote na zidini kusonga mbele kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu, Mweledi na Mwingi wa hekima.
Mwenyezi Mungu akulindeni na akusaidieni.
Sayyid Ali Khamenei
Dei 28, 1394
(Januari 18, 2016).

700 /