Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Sera kuu za Iran ni kushirikiana na nchi za Asia

Katika mazungumzo yake ya alasiri ya leo na Rais Truong Tan Sang wa Vietnam, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiufundi, kibiashara na kiutamaduni kwa ajili ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili na kusema kuwa: "Ushujaa na mapambano ya taifa la Vietnam na shakhsia wake wakubwa kama Ho Chi Minh na Jenerali Giap ambao walikabiliana na kupambana na wavamizi wa kigeni ni jambo ambalo limelifanya taifa la Vietnam liheshimike na liwe na hadhi mbele ya taifa la Iran, na mfungamano huu unapaswa kuandaa mazingira mwafaka ya kuimarisha zaidi uhusiano". 
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria njama za madola makubwa duniani za kutaka kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na kusema: "Uingiliaji huu mara nyingine hufanyika kwa njia ya kuanzisha vita kama vita vya Vietnam na wakati mwingine hufanyika kwa kutumia mbinu nyinginezo; njia ya kukabiliana na uingiliaji huo ni kushirikiana na kukurubiana zaidi nchi zenye misimamo huru." 
Amesema miongoni mwa sera muhimu za Iran ni kushirikiana na nchi za Asia ikiwemo Vietnam. Ameongeza kuwa Vietnam imekuwa ikishirikiana na Iran katika uga wa kimataifa na kwa msingi huo ushirikiano wa nchi mbili unapaswa kuimarishwa zaidi kadiri inavyowezekana. 
Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Rais Hassan Rouhani, Rais Truong Tan Sang wa Vietnam amemshukuru Kiongozi Muadhamu kwa kuenzi mapambano ya wananchi na viongozi wa Vietnam dhidi ya madola ya kigeni na kusema watu wa Vietnam, walipambana na wavamizi wa kigeni kwa miongo kadhaa kwa lengo la kupata uhuru na kujitegemea.
Rais Truong Tan Sang wa Vietnam ameishukuru Iran kwa kuiunga mkono Vietnam katika nyuga za kimataifa. Amesema Vietnam nayo pia inaunga mkono misimamo ya Iran katika uga wa kimataifa na kwamba nchi yake inaamini kwamba kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani ni haki isiyopingika ya Iran na katika siku za usoni Vietnam itaendelea kuiunga mkono Iran.
Amesisitiza udharura wa kuzidishwa ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote na kusema: "Tunatarajia kuwa Iran, katika fremu ya sera zake za kutizama Mashariki, inaitazama Vietnam kama mshirika muhimu, kama ilivyokuwa huko nyuma.
 

700 /