Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa tanzia baada ya kufariki dunia Salahshoor

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe wa tanzia kufuatia kufariki dunia mtengeneza filamu mkubwa na mashuhuri na msanii aliyeshikamana vizuri na dini, marehemu Bw. Farajollah Salahshoor. Matini ya jumbe huo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni hii ifuatayo:

Bismillahir Rahmanir Rahim.
Ninaitumia fursa hii kutoa mkono wa pole kwa familia, jamaa na wafiwa wote wa marehemu Bw. Farajollah Salahshoor; msanii mkubwa aliyeshikamana vizuri na dini. Athari na kazi kubwa na zitakazobakia daima za msanii huyu aliyekuwa na imani thabiti na ambazo zimevuka mipaka ya nchi yetu, ni heshima na fakhari kubwa kwa tasnia ya filamu ya Iran na ni kazi zenye hadhi kubwa mbele ya macho ya mataifa mengine. Bila ya shaka yoyote kazi zake hizo zitampa jazaa njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kulibakisha hai jina lake na wema wake mbele ya watu, Inshaallah.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu ammiminie rehma Zake na maghufira na amnyanyue daraja za juu Kwake mja huyu mwema, na azipe subira nyoyo za wafiwa wote.
Sayyid Ali Khamenei,
8 Isfand, 1394 (Hijria Shamsia)
(27 Februari, 2016 Miladia)

700 /