Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu katika hadhara ya wanafunzi na wanazuoni wa vyuo vya kidini vya Tehran

Ayatullah Khamenei abainisha majukumu matatu makuu ya wanazuoni

Ayatullah Ali Khameni Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran leo (Jumamosi) asubuhi amehutubia umati mkubwa wa wakuu, wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vya kidini vya mkoa wa Tehran na kusema kuwa mwongozo wa kifikra na kidini, mwongozo wa kisiasa na uimarishaji mwamko na mwongozo pamoja na madhuhurio katika Nyanja za huduma za kijamii ni majumu matatu muhimu ya wanazuoni. Amesisitiza kwamba wanafunzi wanapasa kupata mambo yanayofaa na uelewa wa lazima katika dunia ya leo inayozidi kubadilika kwa ajili ya kujitayarisha kutekeleza majukumu muhimu katika jamii. Huku akiwanasihi wanafunzi wa kidini kuthamini thamani na majukumu ya elimu ya kidini, Ayatullah Khamanei ameongeza kuwa hata kama jamii itakuwa na ujuzi wote kamilifu unaohitajika lakini ikakosa kuwa ya kidini, basi itakabiliwa na matatizo makubwa humu duniani na huko Akhera na kwamba jukumu zito la kuibadilisha jamii kuwa ya kidini liko kwenye mabega ya maulamaa, wanazuoni na wanafunzi wa kidini. Amesema maana ya mwongozo wa kidini ni ubainishaji sahihi wa fikra tukufu za Kiislamu. Huku akiashiria athari ya mawasiliano ya intaneti katika kuongeza fikra potovu za kidini na kuwepo nia za kisiasa za kuweka kwenye fikra za vijana fikra potovu na ghalati, Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa medani hii ni medani halisi ya vita na kwamba wanazuoni na wanafunzi wa masomo ya kidini wanapasa kujizatiti na kujitayarisha vilivyo na kuingia katika medani ya kukabiliana na fikra potovu na ghalati. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Uislamu wa kishabiki, kitaasubi, usiozingatia uhakika wa kimaanawi na ulioganda kidhahiri ni mfano halisi wa fikra potovu na kuongeza kuwa katika ncha nyingine ya mkasi huu, kuna Uislamu bandia na wa Marekani ambao unakabiliana na Uislamu halisi.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kudiriki Uislamu halisi na unaotegemea Kitabu na Sunna kwa kutumiwa vyombo vya busara na fikra ya Kiislamu ni jukumu muhimu la wanazuoni na kuongeza kuwa njia ya Manabii ilikuwa ni ya kueneza fikra hii halisi na kwamba wanazuoni pia wanapasa kuendeleza njia hii ya saada, yaani ya kuwaongoza watu kidini. Amesema mwangozo wa kimatendo wa watu unakamilisha mwongozo wao wa kifikra  na kuongeza: Waongozeni watu kwenye ibada na dhahiri pamoja na misdaki za kidini ikiwa ni pamoja na  kusema ukweli, kulinda amana, takwa, kuacha maovu, kuamrisha mema na kukataza mabaya na kuishi maisha sahihi kwa kutumia mbinu bora zaidi. Amesema kuhusiana na suala hilo kwamba imani za kurithiwa za watu zinapaswa kuimarishwa  na kuongeza: Kwa kutumia hoja sahihi, ziimarisheni imani hizo za kurithiwa ambazo huenda zikawa zimepotoshwa kutokana na kupita wakati mrefu na kuzielekeza kwenye njia sahihi. Ayatullah Khemeni amesema mwamko wa kisiasa ni jukumu jingine muhimu la waulama na wanazuoni na kuongeza: Sababu ya kusisitizwa mara kwa mara udharura wa vyuo vya kidini kuwa vya kimapinduzi ni kwamba kudumishwa harakati sahihi na ya kimapinduzi ya nchi na jamii hakuwezekani bila ya kuwepo mahudhurio ya daima ya wanazuoni. Huku akiashiria matukio ya tumbaku, katiba ya masharti na kutaifishwa sekta ya mafuta nchini, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza: Katiba (serikali) ya Masharti na harakati ya utaifishwaji wa sekta ya mafuta hazikufikia malengo yaliyokusudiwa kutokana na kutodumishwa uwepo wa wanazuoni. Lakini uvumbuzi wa Imam Khomeini (MA) ni kwamba hakuruhusu adui asimamishe mahudhurio ya wanazuoni katika harakati kubwa ya Mapinduzi na baada ya hapo. Hii ni kwa sababu kama isingekuwa hivyo Mapinduzi hayangefikia ushindi wala Jamhuri ya Kiislamu kuendelea na harakati zake. Ayatullah Khamenei amesema: Wamarekani tokea mwanzoni mwa Mapinduzi pia kama ilivyo sasa wamekuwa wakifuatilia kufutilia mbali wanazuoni katika harakati kuu ya taifa la Iran ili katika hatua ya baadaye wapate fursa ya kuwaondoa wananchi pia katika medani na hatimaye kuyavunja Mapinduzi, lakini hawajafanikiwa hadi sasa na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa kufikia lengo hilo. Ayatullah Khamenei ameongeza: Katika mtetemeko wa mwamko wa Kiislamu pia dini ilivuta na kuwaleta watu kwenye medani lakini kutokana na kuwa vyombo vya kidini katika nchi hizo zimesimamishwa, jambo hilo halikuweza kuendelea na hivyo mwamko kutofikia natija ya kuridhisha. Ama katika Jamhuri ya Kiislamu, kuendelea kuwepo kwa maulamaa na wanazuoni na hatimaye mahudhurio ya wananchi katika medani yamewezesha kudumishwa kwa harakati ya Mapinduzi. Baada ya kubainisha mwongozo wa kidini na kisiasa, Ayatullah Khamenei amezungumzia jukumu la tatu muhimu la wanazuoni yaani uwepo wao wa kiuongozi na wa kimedani katika utoaji huduma za kijamii. Amesema: Mahudhurio ya wanafunzi wa kidini katika utoaji huduma kwa watu, ujenzi wa shule na mahospitali, kuwasidia watu wanapopatwa na maafa na masuala mengine huwavutia pia watu kujitokeza kwenye medani na hivyo kuwa chanzo cha huduma. Kiongozi Muadhamu amewausia wanafunzi hao wa kidini kusoma vizuri na kutakasa nafsi zao na kusema: Jitahidini kutekeleza vyema majukumu yenu ya kidini, majukumu ambayo hayawezi kutekelezwa na taaluma nyingine yoyote. Bila shaka jambo hilo halipasi kutekelezwa kwa ajili ya kujipatia vyeo, majina na umashuhuri bali wakati wote linapaswa kutekelezwa kwa ajili ya kufikia lengo kuu ambalo ni kumridhisha Mwenyezi Mungu na Imam wa Zama (AF).
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria baadhi ya masuala yaliyozungumziwa na wahadhiri pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kidini vya mkoa wa Tehran na kusema: Suala la kuchungwa vyuo vya kidini visije vikachukua mkondo wa vyuo vikuu, mpango wa masomo ya akhlaki kwenye vyuo vya kidini na kuandikishwa kieneo wanafunzi wa masomo ya kidini ni miongoni mwa majukumu ya wakuu wa vyuo hivyo, masuala ambayo yanapaswa kutekelezwa na kuchukuliwa maamuzi baada ya kuchunguzwa kwa makini.
Kiongozi Muadhamu vilevile ameashiria ukongwe na umuhimu wa vyuo vya kidini vya Tehran pamoja na maulamaa na wanazuoni mashuhuri ambao wamekuwa kwenye vyuo hivyo na kusema: Vyuo vya kidini vya Tehran sasa vina utambulisho ambao unapaswa kuthaminiwa ili kutoa fursa ya kulelewa wanazuoni mashuhuri katika taaluma za fik’hi, taaluma za kiakili, tafisiri na hadithi katika vyuo hivyo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam wal Muslimeen Swadiq Rashad, Mkuu wa Baraza la Vyuo vya Kidini vya Mkoa wa Tehran ameashiria uzoefu wa vyuo vya kidini vya Tehran na mchango wao katika matukio ya kisiasa na kijamii nchini na kusema: Vyuo hivyo vina shule 133, vituo sita vya kitaalamu, wanafunzi 15,000 na wahadhiri 1600. Huku akibainisha kuwa vyuo vya kidini vya Mkoa wa Tehran vimetoa mashahidi 360 kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam wal Muslimeen Rashad amefafanua baadhi ya shughuli na mafanikio ya vyuo hivyo na kusema: Bila shaka moja ya wasiwasi unavikumba vyuo hivi vya kidini ni kuzidi kuwa mbali kwa vyuo hivi na utambulisho wavyo wa asili na kuchukua utambulisho wa vyuo vikuu. Vilevile Mahujjatul Islam wal Muslimeen Swadiqi, Husseini, Panahi, Rouhani, Rastami, Biranovand, Rafii na Panahiyan  pamoja na Mabibi Rasti na Mirmu’mini walitoa mitazamo yao kuhusiana na maudhui mbalimbali zinazowahusu wanafunzi wa kidini na vyuo vya kidini.
Baadhi ya masuala muhimu yaliyozungumziwa na wahadhiri pamoja na wanafunzi hao ni:
-    Udharura wa kuzingatiwa umaanawi katika vyuo vya kidini, kuzingatia akhlaqi na kuarifishwa mifano bora ya kuigwa na kutambulisha mienendo yao ya maisha.
-    Kuzingatiwa vazi la wanafunzi wa kidini, kuwa na moyo pamoja na matendo ya kimapinduzi, kuzingatiwa mapana ya dini na utambuzi wa mahitaji ya zama.
-    Umihimu wa kuwepo mashirikiano baina ya vyuo vya kidini na vyuo vikuu kupitia viti vya fikra huru.
-    Kuimarishwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wanafunzi na wanazuoni na wananchi.
-    Kuarifishwa kwa mpango mkuu wa Bun’yan Marsus kwa lengo la kuimarisha na kufanya kuwa wa kisasa uwezo na utayarifu wa kielimu, kiakhlaqi na kijamii wa wanafunzi.
-    Matatizo ya kimaisha ya wanafunzi na mapendekezo ya kuimarishwa vyuo vya kidini katika maeneo yasiyo ya mijini kwa madhumuni ya kupunguza uhamiaji wa wanafunzi wanaotafuta elimu ya dini.
-    Udharura wa kuwepo mabadiliko ya kimsingi katika mfumo wa masomo katika vyuo vya masomo ya kidini kwa shabaha ya kuimarisha viwango vya elimu na kupunguza kudhoofika kwa motisha na hamu ya kusoma kwa wanafunzi vijana.
-    Kuwepo kwa mafanikio kwa wanafunzi wa kike katika masomo na uhubiri wa maarifa ya kidini na pendekezo la kuasisiwa kituo cha mwanamke wa kijihadi wa Kiislamu kwa lengo la kukabiliana na madhara ya kijamii na kifamilia.
-    Udharura wa vyuo vya kidini kujibu kwa makini na busara fikra potovu na masuala yanayohitajika na jamii kwa kunufaika na misingi imara ya fiqhi halisi.
-    Udharura wa kuanzishwa vituo vya kutoa mafunzo ya kitaalamu kuhusiana na masuala ya uhubiri, utoaji hotuba na ukinaishaji.
Mwishoni mwa hotuba hiyo, swala za Magharibi na Ishaa ziliswaliwa kwa uimamu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 

700 /