Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu aonana na makamanda wa jeshi la polisi

Usalama ni kipaumbele cha kwanza nchini

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi (Jumapili) amehutubia umati mkubwa wa makamanda na wakuu wa jeshi la polisi nchini na kusema kuwa usalama ni suala la daraja ya kwanza nchini na kusisitiza kwamba wakuu wa jeshi hilo wanapasa kusimamia kikamilifu na kwa nguvu zao zote usalama wa kifikra, kimatendo na kimaadili wafanyakazi wa jeshi hilo pamoja na kudhamini usalama wa kijamii na kimaadili. Amesisitiza kwamba mipango yote inapaswa kubuniwa na kupangwa kwa msingi wa akili, mantiki, azma thabiti, uwezo, uzingatiaji sheria na huruma ili sura halisi na inayofaa ya jeshi hilo ipate kuakisiwa kwenye fikra za watu. Kiongozi Muadhamu ameashiria matukio muhimu yaliyojiri nchini katika miezi ya hivi karibuni na kuwashukuru makamanda na wafayakazi wa jeshi la polisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani kutokana na juhudi kubwa walizofanya katika kulinda usalama katika maadhimisho ya Siku Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maandamano ya tarehe 22 Bahman (Februari 11), kufanyika kwa amani na utulivu duru mbili za chaguzi za bunge na la Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu na uwepo wa uwajibikaji wa maafisa wa jeshi hilo katika barabara kuu za nchi wakati wa safari na mapumziko ya mwaka mpya wa Kiirani. Kuhusiana na safari hizo za Norouz, Kiongozi Muadhamu alikumbusha nukta hii kwamba hata kama takwimu zinaonyesha kupungua kwa maafa yanayotokana na ajali za barabarani lakini bado takwimu hizo ziko juu na kwa hivyo jeshi la polisi na idara nyingine husika zinapasa kufanya juhudi zaidi kwa lengo la daima kupunguza idadi ya vifo hivyo.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema maudhui ya usalama ni muhimu sana na ya daraja la kwanza katika vipaumbele nchini na kusisitiza kwamba bila ya kuwepo usalama maisha ya kila siku ya wananchi na shughuli za kielimu za vyuo vikuu, uchumi na uendeshaji wa masuala ya nchi hautawezekana. Amesema, hatua na utekelezwaji wa uchumi ngangari na kumea kwa mti mzuri wa uchumi unaotegemea vyanzo vya ndani pia ni mambo yanayohitajia usalama.
Ayatullha Khamenei amesema kuchunguzwa kwa vyanzo vinavyopelekea kutokuwepo usalama na jeshi la polisi pamoja na idara nyingne husika ni jambo lililo na umuhimu mkubwa na kusisitiza kwamba idara nyingine zote zinapasa kulisaidia jeshi hilo kudhamini usalama nchini. Amesema, usafi (kufaa/ubora), umakini na uwajibikaji wa hali ya juu miongoni mwa makamanda wa daraja la kwanza katika jeshi la polisi na tabia nzuri na ya hisia za ubaba za Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusiana na jeshi hilo ni fursa nzuri ambayo inapasa kutumiwa zaidi kwa ajili ya kufikia malengo yanayokusudiwa. Huku akisisitiza udharura wa serikali kusaidiwa katika kuimarisha viwango na ubora wa jeshi la polisi, Kiongozi Muadhamu ameashiria udharura wa kuwepo misaada ya wananchi kuhusiana na suala hilo na kuongeza: Jeshi la polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani zinapasa kuchunguza kwa makini, kuainisha na kutangaza sehemu ambazo wananchi wanaweza kuingilia kati na kutoa mchango wao katika kuimarisha jeshi hilo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mawasiliano makubwa yaliyopo kati ya polisi na wananchi na kusema kuwa usafi wa jeshi hilo ni jambo lenye umuhimu mkubwa na kuongeza kuwa licha ya kuwa usafi (usalama) wa kifikra, kimatendo na kimaadili katika jeshi la polisi unavutia zaidi uungaji mkono wa wananchi pia unafanya uhusiano wa jeshi hilo na wananchi kuwa wa kirafiki zaidi. Ayatullah Khamenei amesema kuwa usafi huo wa polisi unapatikana kwa sharti la kuwepo usimamizi makini, wa pande zote na wa kudumu na kusisitiza juu ya kuimarishwa na kuenezwa huduma za jeshi la polisi kote nchini na kudhaminiwa usalama katika maeneo yote ya makazi na mazingira wanakoishi watu ikiwa ni pamoja na viunga vya miji, maeneo ya mbali na miji midogo.
Huku akisisitiza kwamba maudhui ya usalama wa kimaadili na madukuduku ya wananchi kuhusiana na suala hilo ni miongoni mwa mambo muhimu ambayo yanapasa kutiliwa maanani na jeshi la polisi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya, uhalifu na uvunjaji wa mila na desturi zilizozoeleka ni mambo yanayohatarisha usalama wa kimwili, kiroho na kimaadili wa jamii na kwa hivyo mipango ya kukaniliana nayo inapaswa kuwekwa kwa kunufaika na mitazamo ya kitaalamu ya wanafikra na wananadharia na hasa wanaotoka kwenye jeshi hilohilo. Ayatullah Khamenei amesema kuhusiana na masuala yanayohusiana na usalama wa kimaadili na baada ya kuwekwa mipango makini na madhubuti, inayokubalika kiakili na sahihi, kwamba upinzani wa baadhi ya watu au uchochezi wa vyombo vya habari kuhusu jambo hilo haupasi kuzingatiwa bali kazi inapaswa kutekelezwa kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu. Amesema kuwepo kwa dhana nzuri kwenye fikra za wananchi kuhusiana na jeshi la polisi ni jambo la dharura na kusisitiza kwamba fikra kuwa polisi ni msaidizi mwenye huruma na aliye na nguvu inapasa kuwekwa kwenye fikra za wanachi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, nguvu na msimamo thabiti ulio na huruma, usafi wa ndani, kufika haraka na kwa wakati eneo la tukio, upole na usaidizi kwa watu na ufuataji sheria ni mambo ambayo huweka picha nzuri kuhusiana na polisi katika fikra za watu. Ayatullah Khamenei amesema kuwa kuthibiti kwa mambo hayo ni uandaliwaji wa mazingira ya kufikiwa maendeleo katika jeshi la polisi na mchango wa jeshi hilo katika maendeleo jumla ya nchi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametathmini maendeleo ya nchi kuwa mazuri na yanayoendelea kupata ufanisi licha ya kuwepo juhudi za miaka 37 za maadui na kuongeza: Kwa kutegemea uungaji mkono wa wananchi, Mfumo wa Kiislamu umeweza kuwadhalilisha maadui na juhudi zao za kuwakatisha tamaa wananchi, kuzua dhana mbaya na hitilafu nchini zinatokana na kukasirishwa kwao na maendeleo ya Iran. Ayatullah Khamanei amewataka viongozi na wananchi wote kuchunga umoja uliopo nchini na kuongeza kuwa kuleta mirengo miwili, makundi mawili na kambi mbili ni miongoni mwa mapigo ya kuangamiza ambayo yanafuatiliwa na maadui. Amesema kuwepo kwa baadhi ya tabia na mienendo miovu kwenye jamii ni kama ilivyo katika nchi nyingine na kuongeza kuwa ili kutathmini kiujumla hali ya Iran, harakati kuu ya wananchi inapaswa kuzingatiwa ambapo Alhamdulillah, harakati hii na mtazamo mpana ni mzuri sana.
Kiongozi Muadhamu pia amesema kuwa shughuli za kitengo cha itikadi na siasa cha jeshi la polisi latika kuimarisha kilaini (taratibu ) motisha ya kidini katika jeshi la polisi ni yenye thamani kubwa na inayopasa kushukuriwa. Pia amezishukuru familia za makamanda na wafanyakazi wa jeshi la polisi ambazo ndizo zinazoandaa uwanja wa kuimarishwa huduma za jeshi hilo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Hussein Ashtari, Kamanda wa jeshi la polisi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitoa mkono wa pongezi na fanaka kwa mnasaba wa kuwadia idi za mwezi mtukufu wa Shaaban na kusema kuwa usimamizi na udhibiti wa mipaka, kuimarisha uwezo wa kukapambana na wahalifu, magaidi, na walanguzi, kuerevusha mifumo, kupunguzwa vifo vinavyotokana na ajali za barabarani, uzingatiaji wa nidhamu katika pande zote, kulindwa kwa nguvu kazi na kusaidia kufikiwa uchumi ngangari ni miongoni mwa mipango na shughuli zinazotekelezwa na jeshi hilo. Jenerali Ashari ameongeza kuwa kujibu madukuduku na matakwa ya wananchi juu ya udharura wa kukabiliana na mienendo miovu na ufisadi ulioratibiwa ni miongoni mwa mipango inayopewa kipaumbele katika jeshi la polisi, mipango ambayo bila shaka inahitajia ufuatiliaji wa kudumu na ushirikiano mkubwa wa mihimili mitatu ya serikali pamoja na idara tofauti nchini.

 

700 /