Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu aonana na rais wa Afghanistan

Kiongozi: Suala la maji ya mito ya mpakani linapasa kutatuliwa

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo alasiri (Jumatano) ameonana na kuzungumza na Rais Muhammad Ashraf Ghani wa Afghanistan pamoja na ujumbe anaoandamana nao ambapo amaeashiria masuala mengi ya pamoja ya kiitikadi, kiutamaduni na kihistoria yaliyopo kati ya mataifa mawili haya ya Iran na Afghanistan. Pia ameahiria suala la mipaka ya pamoja ya nchi mbili na kusisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa na ingali inazingatia kwa makini maslahi na usalama wa Afghanistan na kuamini kuwa maendeleo ya nchi hiyo jirani katika nyanja zote ni maendeleo yake pia. Ayatullah Khamanei amesema kuwa wananchi wa Afghanistan ni watu shujaa, wenye bidii na werevu na kuongeza kuwa Afghanistan ina neema mbili kubwa ambazo ni utajiri wa maliasili na utajiri wa watu ambapo maendeleo makubwa yanaweza kufikiwa kwa kunufaika na utajiri huo. Ameashiria mapokezi mazuri yaliyofanywa na wananchi wa Iran katika miaka ya vita na baada ya hapo na kusema kwamba kinyume na zilivyo baadhi ya nchi zikiwemo za Marekani na Uingereza, Jamhuriya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikiwatazama wananchi wa Afghaistan kwa jicho la heshima, udugu na wenyeji wema na kutosita katika  kuwapa msaada wowote wa kiufundi, kiuhandisi na wa kimiundombinu kwa ajili ya kunufaika na maliasili zao. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza juu ya udharura wa kutatuliwa haraka iwezekanavyo suala la maji ya mito ya mpakani kati ya nchi mbili na kuongeza kuwa masuala kama hayo hayapasi kuwa chanzo cha mvurugiko na malalamiko katika uhusiano wa nchi mbili kama Iran na Afghanistan ambazo zina mpaka, utamaduni na mahitaji ya pamoja.
Katika mzungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bwana Ashraf Ghani, Rais wa Jamhuri ya Afghanistan ameelezea kuridhishwa kwake na mazungumzo ya Tehran na hasa kuhusiana na makubaliano ya kuanzishwa mawasiliano ya uchukuzi na usafiri na India kupitia bandari ya Chabahar na kusema: Sisi daima hushukuru mapokezi mazuri ya wananchi wa Iran  na mtazamo wako mzuri kuhusiana na Afghanistan na tunatumai kwamba uwanja wa kuimarishwa zaidi uhusiano wa pande mbili utaandaliwa kufuatia mazungumzo ya Tehran. Bwana Ashraf Ghani ameendelea kusema: Wiki ijayo, kikao cha wataalamu kitafanyika kuhusu masuala yanayohusiana na matumizi ya pamoja ya nchi mbili ya maji ya mito ya mpakani na tunatumai suala hili litatatuliwa kwa njia inayofaa.

 

700 /