Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu akutana na washairi

Watu wafahamishwe hiana ya Marekani kuhusu JCPOA

Katika usiku wa kumkia siku ya kuzaliwa Imam Hassan al-Mujtaba (as), kundi la wanautamaduni, wahadhiri wa mashairi na fasihi ya Kifarsi, washairi vijana na wakongwe nchini pamoja na washairi kadhaa kutoka nchi za Pakistan, India na Afghanistan wamekutana na Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika mkutano huo, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa washairi ni rasilimali na akiba kubwa kwa nchi na huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mashairi kuwa hai, kuendena na wakati na kuwa na msimamo kuhusiana na masuala muhimu na mahitaji ya nchi, amesema: ‘Leo kuna vita vingine (vipya) vinavyoendelea kwa anwani ya vita laini na mapambano ya kisiasa na kiutamaduni na washairi wakiwa chombo chenye athari kubwa wanapasa kutekeleza majukumu yao katika uwanja huu.’ Ayatullah Khamenei amesifu na kumuenzi mshairi marehemu Hamid Sabzawari kutokana kipawa chake kikubwa alichokuwa nacho katika mashairi na ujuzi pamoja na ubunifu wake mpana wa matumizi ya maneno na kusema: ‘Sifa isiyo na mfano wake ya marehemu Sabzawari ni nyimbo zake zilizokuwa na taathira, ubora na zilizoendana na wakati.’ Kuhusu suala hilo, Ayatullah Khamenei amesema kwamba nyimbo ni aina iliyo na taathira kubwa zaidi ya mashairi na kuongeza kuwa kasi na upana wa watu kujifunza nyimbo ni mkubwa zaidi kuliko aina zote za mashairi. Amesema nyimbo kama ulivyo upepo mwanana wa msimu wa machipuo, hupenya kirahisi kwenye jamii, na hivyo juhudi zinapasa kufanyika kwa madhumuni ya kutunga nyimbo nzuri na kuzisambaza vizuri ili kuondoa mapungufu na kujaza mapengo yaliyopo kwenye uwanja huu.
Ayatullah Khamenei kisha amebainisha nafasi na jukumu la Mashairi na kusema kuwa washairi ni sehemu ya rasilimali bora na ya fahari zaidi nchini na kuongeza kuwa rasilimali hiyo inapasa kutumika katika vipindi ambavyo nchi inahitajia msaada katika masuala kama vile ya kisiasa, kiutamaduni, mawasiliano ya wananchi, viunganishi vya kijamii na kupambana na maadui wa nje. Amesema rasilimali hii inapasa kuletwa kwenye medani na kukidhi mahitaji ya nchi.
Kiongozi Muadhamu amesisitiza: ‘Mashairi yanapasa kuwa hai na kuchukua msimamo kuhusiana na masuala yanayoendelea nchini na mahitaji ya nchi.’ Huku akisisitiza juu ya udharura wa kuenezwa mashairi na nyimbo hai na zilizo na msimamo wa wazi katika upeo mpana na majukumu ya Shirika la Idhaa na Televisheni ya Taifa  na idara nyinginezo husika katika uwanja huo, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: ‘Kinyume na ilivyokuwa huko nyuma leo mashairi hai na muhimu yanasomwa kuhusiaa na masuala kama vile  Palestina, Yemen, Bahrain, kujihami kutakatifu, mashahidi wapiga mbizi, mashahidi walinzi wa Haram takatifu za Kizazi cha Mtume (saw) au kuhusu kudhulumiwa mujahidina kama vile Sheikh Zakzaky, mwanazuoni madhlumu, shujaa na aliye na azma thabiti wa Nigeria, lakini kwa bahati mbaya mashairi haya yenye taathira na ya kutia moyo hayaenezwi na kuakisiwa kama inavyotakiwa, na kuna kasoro na upungufu mkubwa katika uwanja huu.’ Ayatullah Khamenei amesema kubainishwa hiana za Wamarekani kuhusiana na kadhia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni uwanja mwingine ambapo mashairi hai yanaweza kusomwa na kuongeza kuwa mbali na wanasiasa, wasanii na hasa washairi wanapasa kuwaakisia watu ukweli huu. Huku akikosoa baadhi ya hatua ghalati zinazochukuliwa katika kueneza na kuwaenzi wasanii wasiokuwa na itikadi wala kujali, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: ‘Kwa bahati mbaya mara nyingine mtu asiyekuwa na muelekeo wowote wa maarifa ya Kiislamu wala Mapinduzi ya Kiislamu huenziwa lakini yule msanii ambaye ametumia umri wake wote na rasilimali yake ya kisanii katika njia ya Uislamu na Mapinduzi huwa haenziwi wala kupewa umuhimu.’ Nasaha nyingine ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ilikuwa ni kunufaika na fursa ya kuvutiwa na kuzingatia watu na vijana mashairi yanayotumika sana kama vile ya tahalili (maombolezo) na utenzi. Ameashiria mifano ya tahalili zenye madhumuni muhimu na ya hamasa katika kipindi cha mapambano ya wananchi dhidi ya utawala wa kitaghuti nchini Iran na vilevile katika kipindi cha vita vya kujitetea kutakatifu nchini na kusema: ‘Ni wazi kuwa medani na aina ya vita vya leo vinatofautiana na vile vya kipindi cha mapambano na miaka ya mwanzoni mwa Mapinduzi, ambapo sisi hii leo tuko kwenye medani ya vita laini, vya kisiasa, kiutamaduni, kiusalama na mapambano dhidi ya upenyaji, ambapo katika medani hii ni fikra na irada ndizo zinazopambana na mojawapo ya zana za msingi na zenye taathira katika mapambano hayo pia ni zana ya mashairi.’ Sisitizo juu ya utungaji, kutarjumiwa na kusambazwa kimaudhui mashairi muhimu kuhusu masuala kama vile ya Palestina, vita vya kujitetea kutakatifu, masuala ya kieneo, Yemen, kubadilishwa kwa madhumuni na maneno matukufu ya dua na maandiko ya kidini kwenye mashairi na kuimbwa mashairi muhimu ya kidini na yaliyo na madhumuni aali kwa lengo la kueneza maarifa na mafundisho ya Maimamu watukufu na maasumu (as) ni nasaha nyingine alizotoa Kiongozi Muadhamu katika kikao hicho cha kirafiki na washairi.
Ayatullah Khamenei vilevile amesisitiza udharura wa kuimarishwa na kuboreshwa mashairi na kutosimama bila harakati washairi katika njia ya maendeleo. Amesema: ‘Vyombo vya umma na ufundi vinapasa kuimarishwa na kuungwa mkono kwa lengo kunyanyuliwa kiwango cha mashairi na mafunzo ya washairi nchini.’
Mwanzoni mwa kikao hicho washairi 23 walisoma mashairi yao mbele ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Washairi vilevile waliswalishwa na Kiongozi Muadhamu swala za Magharibi na Ishah na kisha kufuturu pamoja naye baada ya kuwa wamefunga mchana kutwa.

 

700 /