Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi akutana na baraza la mawaziri

Hatua kali zichukuliwe dhidi ya mishara mikubwa ya kupindukia

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo (Jumatano) alasiri amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu pamoja na baraza lake la mawaziri na kuzungumzia nukta kadhaa za maneno ya hekima ya Imam Ali (as) kutoka kitabu cha Nahjul Balagha. Huku akiashiria baadhi ya maneno ya Imam Ali (as) kuhusiana na hatua ya kuchukuliwa katika hali ya fitina, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa Amir al-Mu’mineena Ali (as) ananasihi kuwa katika mazingira ya fitina ambapo huwawia watu vigumu sana kutenganisha kati ya haki na batili, tunapasa kufanya mambo kwa namna ambayo haitakuwa na manufaa yoyote kwa fitina. Amesema katika mazingira ya fitina kama yale ya mwaka 1388 (2010) wa Kiirani, hatupasi kutoa matamshi, kukaa kimya, kuchukua hatua au hata kutoa ishara inayoipa nguvu fitina.
Ayatullah Khamenei ameongeza: ‘Bila shaka kuna baadi ya watu ambao kutokana na mitazamo yao mahususi huenda wasiwe na hamu ya kusimama moja kwa moja mbele ya fitina lakini pamoja na hayo watu hao (msimamo wao) hawapasi kutumika kwa manufaa ya fitina.’ Ameashiria usemi mwingine  wa hekima kati ya semi za hekima za Imam Ali (as) kwenye Nahjul Balagha kuhusiana na suala la vyeo kutochukuliwa kuwa fursa ya kujikusanyia utajiri na kujinufaisha kwa njia maalum na kusema: ‘Mtazamo kama huo kuhusu cheo ambacho kwa hakika ni amana humpunguzia mtu hadhi na kumdhalilisha.’ Kuhusu suala hilo Kiongozi Muadhamu ameashiria suala la hivi karibuni la mishara mikubwa ya kupindukia na kusema kuwa suala hilo kwa hakika ni hujuma dhidi ya thamani. Hata hivyo amewataka watu wote kufahamu kuwa suala hilo linashuhudiwa kwa watu wachache sana na kwamba wakurugenzi na wasimamizi wengi wa idara za serikali ni watu wema. Pamoja na hayo amesema suala hilo ni baya sana na kutaka hatua kali zichukuliwe ili kukabiliana na watu wanaopokea mishara mikubwa kupindukia. Ameashiria amri ya hivi karibuni ya Rais Hassan Rouhani kwa makamu wake wa kwanza kwa lengo la kufuatilia na kuchukuliwa hatua dhidi ya suala hilo na kusema kuwa suala hilo halipasi kufungamanishwa na wakati bali linapasa kufuatiliwa kwa bidii na wananchi kufahamishwa matokeo yake. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: ‘Kwa mujibu wa habari zilizonifikia, mishahara ya wakurugenzi katika idara nyingi ni ya kiwango kinachokubalika na mishahara mikubwa inahusiana na idadi ndogo sana ya wakurugenzi ambapo idadi hii ndogo ndiyo inayopasa kuchukuliwa hatua kali.’
Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei ameashiria hekima nyingine ya Imam Ali katika Nahjul Balagha na kusema: ‘Daima tunapasa kuchunga ndimi zetu, kwa sababu matatizo mengi ya mwanadamu yanatokana na ulimi wake.’ Amesisitiza kwamba baadhi ya wakati matatizo yanayotokana na kutochunga ulimi huwa ni ya mtu binafsi lakini wakati mwingine huwa ni ya kijamii na kwa hivyo tunapasa kuwa waangalifu mno kuhusiana na suala hilo.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu, Rais Hujjatul Islam wal Muslimineen Hassan Rouhani alitoa ripoti kuhusu shughuli na hatua muhimu zaidi ambazo zimepigwa na serikali kufikia sasa. Mwishoni mwa kikao hicho swala za Maghrib na Ishaa ziliongozwa na Kiongozi Muadhamu na kisha waalikwa kufungua swaumu yao kwa dhifa ya futari wakiwa na Kiongozi Muadhamu.

 

700 /