Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi akutana na mabalozi wa nchi za Kiislamu

Kusahaulika Palestina, lengo kuu la njama za Marekani katika eneo

Leo nchana (Jumatano), Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonana na kuzungumza na wakuu wa Mfumo wa Kiislamu na matabaka tofauti ya wananchi ambapo amesema kuwa chanzo halisi cha vita, ukosefu wa usalama na ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu ni madola ya kiistikbari yanayoongozwa na Marekani. Huku akisisitiza kwamba lengo lao kuu ni kuuandalia utawala haramu wa Israel mwanya wa kupumua na wakati huohuo kuusahaulisha ulimwengu suala muhimu la Palestina, Kiongozi Muadhamu amesema kwamba njia pekee ya kupambana na njama hizo ni kumfahamu vyema adui halisi na kusimama imara mbele yake na kuongeza kuwa taifa la Iran limethibitisha kwamba njia pekee ya kufikia maendeleo ni kusimama imara. Huku akiwapongeza Waislamu kwa mnasaba wa kuwadia Siku Kuu ya Idul Fitr, Ayatullah Khamenei ameashiria matukio ya hivi sasa katika ulimwegu wa Kiislamu, mauaji ya kutisha, kutokuwepo usalama na milipuko ya kigaidi inayotokea mara kwa mara katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema: ‘Moja ya masuala muhimu ni kufahamu vyema chanzo kiovu cha matatizo yanayoukumba Umma wa Kiislamu hii leo na mikono miovu ya siri ambayo inaeneza ugaidi.’ Ayatullah Khamenei ameashiria matangazo yanayotolewa na nchi zote ya kulaani na kujitenga kidhahiri na ugaidi na wakati huohuo kubuni miungano bandia ya eti kupambana na ugaidi na kusema: ‘Licha ya madai ya kidhahiri yanayotolewa na madola hayo kuhusu ugaidi, lakini ndiyo yanayoeneza na kuunga kivitendo ugaidi huo.’ Ameashiria kushiriki  moja kwa moja kwa balozi wa Marekani katika mijimuiko ya wapinzani wa serikali ya Syria katika siku za mwanzoni za matukio ya Syria na kuandaliwa mazingira ya kugeuzwa mzozo wa kawaida wa kisiasa wa nchi hiyo kuwa vita vya ndani, na kusema: ‘Waliubadilisha mgogoro wa kisiasa na kuwa mauji ya ndugu kwa ndugu na kisha kupitia uungaji mkono wa silaha na fedha na mapato haramu ya mafuta, walitoa watu katika sehemu tofauti na kuwapeleka Syria na Iraq na kuzua ukosefu wa usalama na matatizo ambayo tunayashuhudia hii leo katika eneo.’ Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uadui usiokoma wa Marekani dhidi ya taifa la Iran na kusema kuwa unatokana na uzoefu wa miaka 37 na utambuzi wa taifa hili na kuongeza: ‘Marekani tokea mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ilianzisha uadui dhidi ya Imam Mpendwa (MA) na harakati yake kubwa ambapo uadui huo ungali unaendelea hadi leo lakini njama hizo za Marekani zimeshindwa kufua dafu kutokana na mwamko wa serikali na utayarifu wa viongozi.’ Huku akisisitiza kwamba Umma wa Kiislamu unahitaji kumfahamu vyema adui pamoja na njama zake, Ayatullah Khamenei amesema: ‘Tunashuhudia mfano mwingine wa kubadilishwa mvutano wa kisiasa kuwa vita vya ndani huko Bahrain.’ Amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiingilii  na wala haitaingilia kwa vyovyote vile masuala ya ndani ya nchi hiyo lakini kwamba kama kuna ufahamu na busara yoyote ya kisiasa nchini humo watawala wa nchi hiyo hawapasi kuacha mvutano huo wa kisasa kugeuka na kuwa vita vya ndani wala kuruhusu wananchi kupigana. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba lengo kuu la njama za uistikbari wa kimataifa ukiongozwa na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ni kutaka kulifanya suala la Palesytina lisahaulike na kuongeza kuwa wanataka kukana kuwepo kwa jiografia na taifa la Palestina katika hali ambayo Palestina ina historia kongwe ya maelfu ya miaka na kwamba taifa la Palestina ni taifa lililo na ardhi, ukweli ambao hauwezi kukanushika. Atyatullah Khamenei amesisitiza kwamba bila shaka utawala haramu wa Kizayuni utapata pigo kutokana na mashinikizo unayoyatoa dhidi ya taifa dhulumiwa na lililo chini ya mzingiro la Palestina. Ameongeza kuwa suala la Palestina ni suala la msingi katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba hakuna nchi yoyote ya Kiislamu na hata zisizo kuwa za Kiislamu lakini ambazo zina utu, zinazopasa kulisahau suala hili. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia hali inayotawala nchini Yemen na kushambuliwa kila siku kwa mabomu nyumba za raia, mahospitali, misikiti na miundombinu ya nchi hiyo na kusisitiza kwamba mchokozi anapaswa kukomesha uchokozi wake huo na ulimwengu wa Kiislamu pia kumuadhibu mchokozi huyo ambaye anawahujumu wananchi wa Yemen kwa sababu zisizo na msingi wowote.
Huku akiashiria ukakamavu na msimamo imara wa wananchi wa Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: ‘Maendeleo ya Iran ya Kiislamu yanatokana na mapambano na kama taifa la Iran lingeamua kusalimu amri mbele ya madola yenye nguvu bila shaka lisingepata maendeleo ya hivi sasa.’ Amesema ukakamavu, mapambano, kuimarisha uzalishaji wa ndani, azma na irada ya kitaifa na kumtegemea Mwenyezi Mungu ni masuala muhimu yanayodhamini kufikiwa maenedeleo na kuongeza: ‘Iwapo taifa lolote lile litakuwa kakamavu kutokana na imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu tu bila ya kumuogopa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, bila shaka litapiga hatua kuelekea kwenye malengo yake matukufu.’
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Dakta Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa pongezi na fanaka wa Idul Fitr na kusema kuwa ugaidi, machafuko na ukimbizi ni miongoni mwa matatizo muhimu yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu hii leo na kusisitiza juu ya udharura wa kubuniwa muungano halisi kwa ajili ya kupambana na ugaidi badala ya miungano bandia na ya kidhahiri tu. Ameendelea kusema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama ilivyokuwa huko nyuma, itaendelea kushughulikia kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu na kutatetea mataifa ya Kiislamu. Dakta Rouhani vilevile ameashiria suala la mishahara ya kupindukia na kusema: ‘Ikishirikiana na mihimili mingine ya dola, serikali imeazimia kutatua tatizo hilo kwa uugaji mkono wa wananchi na Kiongozi Muadhamu. Amesema, mbali na kuchukuliwa hatua za haraka, uwazi na marekebisho ya sheria yanapaswa kufanywa ili kuzuia kukaririwa kwa kesi kama hizo na serikali itawasilisha bungeni mswada kuhusiana na suala hilo.’

700 /