Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika Swala ya Udul Fitr

Mishahara haramu ni matokeo ya kuenezwa ubwanyenye nchini

Wananchi wacha-Mungu wa Iran leo (Jumatano) wameswali Swala ya Idul Fitr kote nchini ikiwa ni katika kumshukuru Mwemyezi Mungu kwa kuwapa fursa ya mwezi mzima kwa ajili ya kufanya ibada. Kilele cha swala hiyo ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kilishuhudiwa katika Mswala wa Imam Khomeini mjini Tehran ambapo Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliswalisha swala hiyo. Katika hotuba ya kwanza ya swala, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwapongeza wananchi wa Iran na Umma mzima wa Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia Siku Kuu hii muhimu ya Waislamu na kusema kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu nchini ulijaa umaanawi, uzingatiaji, kutawasali, unyenyekevu na dua na kuongeza: ‘Sisi viongozi tunapasa kuzihusudu nyoyo zilizojaa nuru na mwanga za wananchi, na bila shaka kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, lakini kwa upande mwingine tunapasa kutambua uzito wa makujumu tuliyonayo kuhusiana na wananchi hawa waumini nchini.’ Ayatullah Khamanei amesema kuwa watu, hasa tabaka la vijana kufunga Saumu katika siku hizi ndefu na zenye joto jingi zaidi ni miongoni mwa matukio ya kuvutia ya mwezi wa Ramadhani mwaka huu na kuongeza kuwa bila shaka mikono khabithi ilijaribu kuwafanya vijana wasifunge lakini kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu haikufanikiwa na haitafanikiwa pia katika siku zijazo. Amesema kuwa suala hilo linapasa kuwafanya wananchi na viongozi watambue ni mipango gani waliyonayo maadui khabithi wa Iran ya Kiislamu kwa ajili ya kukiweka mbali kizazi kinachoinukia cha vijana na dini, lakini hata hivyo mipango ya mwaka huu ya waovu hao ilishindwa kutokana na mwamko wa watu. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kufanyika maandamano makubwa ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika joto kali na hasa katika mikoa ya kusini mwa nchi, ni dhihirisho jingine la kuvutia na moja ya kazi muhimu zilizotekelezwa na wananchi kutokana na mapambano na ukakamavu wao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa kwa mahudhuria yao hayo makubwa na kupaza sauti zao kuhusiana na suala la Palestina, kwa hakika wananchi wametangaza wazi kwamba hata kama baadhi ya serikali za Kiislamu zimeyafanyia hiana malengo matukufu ya taifa la Palestina, baadhi ya serikali kuzembea au baadhi ya mataifa kughafilika na suala hilo lakini taifa la Iran liko macho na kusimama imara mbele ya maadui wote kwa ajili ya kuhuisha suala la Palestina. Ayatullah Khamenei amesema kwamba mwezi wa Ramadhani mwaka huu, yalikuwa ni maonyesho makubwa ya madhihirisho na viashiria vya umaanawi wa wananchi na kugusia vikao muhimu mbalimbali vya usomaji Qur’ani ambavyo vilifanyika katika Haram Takatifu tofauti nchini na kuakisiwa kwa njia ya kuvutia mno na Shirika la Kitaifa la Utagazaji IRIB. Ameongeza: ‘Moja ya madhihirisho hayo ni dhihirisho hili linaloenea nchini la kuandaliwa futari za umma katika miji tofauti na hasa katika maeneo tofauti mjini Tehran ambapo umaanawi huu wa kuwa na moyo wa kuwahudumia watu kwa hakika ni jambo linalomvutia kila mtu mwenye insafu.’ Amesema dhihirisho hili zuri na la kuvutia la kuandaliwa futari za umma ni kinyume na futari nyinginezo za kujifaharisha ambako isirafu kubwa hufanyika. Ameongeza kwamba kwa bahati mbaya baadhi ya idara hujihusisha na jambo hili baya la kuwaandalia watu wasiostahiki futari ghali kwenye mahoteli, ambapo tunapasa kusema kuna futari za kawaida kabisa za umma ambazo huandaliwa watu wanaostahiki na wapita njia, mkabala na suala hili. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kutawanywa futari kwenye nyumba za wahitaji na vijana wanaojiita ‘vikosi vyenye hamu vya mtaani,’ kuandaliwa kwa vikao vya kuvutia vya usomaji Qur’ani na dua misikitini, husseiniya na makaburi ya mashahidi na hasa katika nyusiku za Lailatul Qadr, suna inayoenea na iliyo na baraka ya kufanya itikafu katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani na hatua ya baadhi ya madaktari ya kutoa bure huduma za tiba katika mwezi huu mtukufu ni miongoni mwa mambo ya kuvutia ambayo yalishuhudiwa katika mwezi huu mtukufu na kusisitiza kwamba Ramadhani kama hii bila shaka huvutia rehema za Mwenyezi Mungu.
Katika hotuba yake ya pili katika Swala ya Idul Fitr, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria milipuko ya kigaidi iliyotekelezwa na magaidi wa Daesh katika siku za hivi karibuni  huko Iraq, Uturuki na Bangladesh na nchi nyinginezo na kusema: ‘Kwa bahati mbaya mwaka huu Idul Fitr ya Waislamu katika baadhi ya nchi ilibadilika na kuwa ya maombolezo kutokana na vitendo vya magaidi ambao kwa amri ya mabwana zao, wanataka kuubadiisha Uislamu halisi na Uislamu bandia, na jinai hii ni matokeao ya magaidi kupewa mafunzo na vyombo vya ujasusi vya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni.’ Huku akisisitiza kwamba jukumu la mauaji ya watu wasio na hatia katika eneo linapaswa kubebwa na waungaji mkono wa ugaidi huo wa kitakfiri, ambapo hata hivyo amesema kuwa waungaji mkono hao sasa taratibu wameanza kuonja madhara ya ugaidi huo, lakini Kiongozi Muadhamu amesema kwamba dhambi na uhalifu wao huo hautasahaulika. Amesikitishwa na kuashwa moto wa vita na ghasia katika nchi za eneo zikiwemo Syria, Libya na Yemen na kusema ni mwaka mmona na miezi mitatu sasa ambapo wananchi wa Yemen wanashambuliwa kwa mabomu lakini kwamba wananchi hao na viongozi wao wenye busara wanapaswa kupongezwa kwa kufanya maandamano makubwa ya Siku ya Kimataifa ya Quds katika mazigira kama hayo na joto kali. Huku akisema kwamba lengo kuu la madola ya kiistikbari kuanzisha vita, machafuko na ugaidi katika eneo ni kutaka kusahaulisha suala la Palestina, Ayatullah Khamanei amesema mapambano kwa ajili ya kukombolewa Palestina ni mapambano ya Kiislamu na ya watu wote ambapo kudumishwa kwa mapamano hayo ni jukumu la Waislamu wote na kwamba ni makosa makubwa kulichukulia suala la Palestina kuwa ni suala la ndani na Kiarabu tu.
Akiwa mwishoni mwa hotuba ya pili ya Swala ya Idul Fitr, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria suala la mishahara na malipo yasiyo ya insafu na ya kidhulma na kusema kuwa mishahara na kuchukuliwa kusiko halalishwa kwa pesa kama hizo kutoka Beitulmal ni dhambi na hiana dhidi ya malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu. Ameendelea kusema kuhusu suala hili kwamba bila shaka makosa na uzembe ulifanyika huko nyuma ambapo ufidiaji unapasa kufanywa. Amesisitiza kwamba viongozi wanapasa kufuatilia kwa karibu suala la mishahara haramu na kwamba isiwe kuwa makelele mengi yanapigwa baada ya kufichuliwa suala kama hilo na kisha kusahaulika na hali kurejea katika hali ya kawaida baada ya kupita wakati.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewasifu rais wa nchi na wakuu wengine wa mihimili miwili ya dola yaani bunge na vyombo vya mahakama kutokana na misimamo yao thabiti ya kufuatilia kwa karibu suala hili ovu na kusema: ‘Kuhusu suala hili mishahara isiyohalalishwa inapaswa kurejeshwa na watu waliokiuka sheria kuadhibiwa na wale waliotumia vibaya sheria pia kufutwa kazi, kwa sababu hawafai kuwa kwenye nafasi za kiidara na uongozi.’
Huku akisisitiza kwamba maadui wa Mfumo wa Kiislamu wanafanya juhudi za kutumia vibaya suala hili dhidi ya Mfumo, Ayatullah Khamanei amesema kwamba idadi ya watu waliopokea mishahara hiyo isiyo halali ni ndogo mno ikilinganishwa na ya maafisa wasafi na wema wa Mfumo, na kwamba licha ya hayo lakini idadi ndogo hiyo pia ni madhara na kasoro ambayo inapaswa kuondolewa. Amesema moja ya sababu za kudhihiri maovu ya mishahara isiyo halali ni madhara yanayotokana na ubwanyenye na kusisitiza kuwa wakati ubwanyenye, israfu na anasa vinapoenea kwenye jamii matokeo yake huwa ni kudhihiri kwa maovu kama vile ya mishahara haramu. Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kw amara nyingine tena amesisitiza udhahrura wa kupambana na jambo hilo na kusema suala la kufutwa kazi na kurudishwa fedha kwenye Baitulmal linapaswa kuwekwa kwenye ajenda ya viongozi kwa sababu fikra za waliowengi nchini zinashughulishwa na suala hili na kuwa iwapo halitafuatiliwa kwa karibu imani ya wananchi kwa Mfumo wa Kiislamu itapungua. Ayatullah Kahamenei amesema kupungua imani ya wananchi kwa Mfumo wa Kiislamu ni msiba na maafa makubwa na kusisiza kwamba viongozi wanapasa kulinda imani hii ya wananchi kwa kufuatilia kwa karibu na kuchukua hatua muhimu.

 

700 /