Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Adui atambue kuwa, akishambulia atapata kipigo kikali

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, adhuhuri ya leo (Jumapili) amehutubia hadhara ya makamanda na maafisa wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amesisitiza umuhimu wa ulinzi huo na kuutaja kuwa ni mstari wa mbele katika mapambano ya kukabiliana na mashambulizi yoyote. Amesema kuwa, kambi inayokabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ni kambi ya watu makhabithi, walaghai na wapinzani wa uhuru na kujitawala taifa la Iran. Ameongeza kuwa: Katika kukabiliana na adui wa namna hii ambaye lengo lake ni kudhoofisha uwezo na nguvu za kiulinzi cha nchi yetu, kuna ulazima wa kuviimarisha ipasavyo vikosi vyetu vya jeshi la ulinzi kwa kadiri kwamba adui hatakuwa hata na fikra ya kuishambulia nchi yetu. 
Ayatullah Khamenei amesema azma, irada ya kweli na uwezo wa nguvu ya kibinadamu ni mambo muhimu ya kuondoa vizingiti na udhaifu wa aina mbalimbali. Ameongeza kuwa kituo cha ulinzi wa anga ni sehemu ya mstari wa mbele na asili na kuna udharura wa kudhoofisha azma ya adui ya kutaka kuihujumu Iran kwa kuthamini nafasi hiyo muhimu na kuonesha azma na irada imara.  
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, uadui dhidi ya taifa la Iran na dhidi ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mkubwa zaidi ikilinganishwa na uadui unaojulikana leo duniani baina ya nchi na mataifa mbalimbali. Ameongeza kuwa: "Kambi itunayokabiliana nayo ambayo tunaiita mfumo wa ubeberu au Uzayuni wa kimataifa ni kambi ya watu makhabithi, walaghai na wenye fikra za kidhalimu ambao uadui wao ni dhidi ya itikadi za kidini, uhuru na kutokubali kuburuzwa taifa la Iran.
Amesema uadui wa kambi hiyo unadhihirishwa kwa sura mbalimbali na kuongeza kuwa: Wakati mmoja uadui huo unadhihirika kwa sura ya Marekani na siku nyingine kwa sura ya utawala wa kidhalimu kama ule wa Saddam, lakini lililo muhimu ni kuwa, Iran inapaswa kuchukua misimamo na maamuzi sahihi na kuyafanyia kazi kivitendo kwa kutumia suhula na uwezo wake mmkubwa pamoja na kuelewa vizuri zama za sasa na mipango ya adui.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, upinzani na makelele mengi yaliyozushwa kuhusu mfumo wa kujilinda kwa mokombora wa S-300 au taasisi unayolindwa ya Fordow ni miongoni mwa mifano ya wazi ya ukhabithi wa adui wa taifa la Iran. Ameongeza kuwa: Mfumo wa makombora wa S-300 ni mfumo wa kujilinda na kujihami na si mfumo wa kushambulia, lakini pamoja na hayo Wamarekani wamefanya njama zote kuzuia Iran ipate mfumo huo.
Amesema: "Sisi tunakabiliwa na adui wa aina hii ambaye hataki hata tufaidike na haki yetu ya kujilinda na kwa hakika wanasema kaeni bila ya ulinzi ili wakati wowote wanapotaka kuishambulia nchi yetu waweze kufanya hivyo.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran vilevile ametilia mkazo udharura wa kuwa macho, kuchukua hatua kwa wakati unaofaa na kutumia mbinu za aina mbalimbali pamoja na silaha za kisasa za ulinzi wa anga na kusisitiza kuwa: Adui anapaswa kuelewa kuwa kama atatushambulia basi atapata pigo kubwa na kwamba kujihami kwetu huko kutaambatana na majibu.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Farzad Ismaili, kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya SAW ametoa hotuba fupi na sambamba na kuenzi maadhimisho ya mwaka wa nane wa kuanzishwa kituo hicho ametoa ripoti fupi kuhusiana na hatua muhimu zaidi zilizochukuliwa na kituo hicho hadi hivi sasa.
 

700 /