Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Khamenei:

Jeshi la Iran linapaswa kuwa tayari wakati wowote

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi (Jumatano) amehudhuria sherehe za kuhitimu masomo, kula viapo na kupandishwa cheo wanachuo wa vyuo vikuu vya maafisa wa kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilizofanyika katika chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga cha Shahid Sattari.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitizia wajibu wa kujiimarisha na kujiweka tayari wakati wote vikosi vya ulinzi vya Iran katika upande wa kiitikadi, kielimu na kinidhamu, na kuwarithisha vijana uzoefu wa vita vya kujihami kutakatifu (vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa zamani wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ilikuwa ndio kwanza imeanzishwa wakati huo.(
Aidha amebainisha kuwa, leo hii taifa la Iran linakabiliana na kambi kubwa ya adui kutokana na kushikamana kwake na Uislamu, uhuru na matukufu yake makuu na kuongeza kwamba: Kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu ulikuwa mtihani mzito ambao ndani yake, johari ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilionekana wazi kwani lilifanya kazi kubwa zinazong'ara.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kwa hakika vita hivyo vya kulazimishwa vya miaka minane, vilikuwa vita vya kimataifa na ni mashambulizi ya pande zote ya madola makubwa duniani na mabarakala wao wa kieneo na kimataifa, na kwamba mashambulizi hayo yalilenga kuangamiza mipaka, utambulisho, matukufu na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Mapinduzi ya taifa la Iran.
Ayatullah Khamenei amesema, moja ya hatua za dharura katika vyuo vikuu vya vikosi vya jeshi la ulinzi la Iran ni kutoa elimu kuhusu kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu na kuwabainishia vijana hali ilivyokuwa wakati huo. Amesisitiza kuwa: Leo hii, dunia nzima, marafiki na maadui wanaikiri adhama, welewa, ushujaa na nguvu za taifa la Iran na za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Amirijeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Iran aidha amewaenzi makamanda na maafisa wakuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa weledi wao, jihadi na kujitolea kwao katika njia ya haki.
Vilevile Ayatullah Khamenei amekaguwa gwaride na vikosi mbalimbali vya kijeshi vilivyoshiriki kwenye sherehe hizo.
 

700 /