Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Utawala wa Kizayuni unataka kudhoofisha uhusiano wa Iran na Azerb

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa dini ya Uislamu ni sababu kuu inayoifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ijihisi kuwa na ukuruba na udugu na watu na viongozi wa Azerbaijan.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo alasiri ya leo (Jumapili) wakati alipofanya mazungumzo na Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan aliyeko safarini hapa nchini. Ameongeza kuwa, kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi cha pande hizo mbili kiko chini sana ikilinganishwa na uwezo wa nchi hizi mbili na kwamba biashara baina ya Iran na Azerbaijan inapaswa kuongezeka mara kumi zaidi ya kiwango cha sasa.
Ayatullah Khamenei amepongeza misimamo ya serikali ya Azerbaijan kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa ni pamoja na misimamo ya Baku katika mazungumzo ya nyuklia na kusema: Serikali ya Azerbaijan daima imekuwa bega kwa bega na Iran katika duru za kimataifa na misimamo hiyo mizuri inazikurubisha zaidi nchi hizo mbili.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria hasira ya maadui kutokana na uhusiano wa karibu wa Iran na Azerbaijan na kusema: Utawala habithi wa Israel unafanya jitihada kubwa zaidi za kudhoofisha uhusiano wa kidugu wa Iran na Azerbaijan kuliko maadui wengine wote na kwa msingi huo kuna ulazima wa kulindwa uhusiano mzuri uliopo.
Vilevile amepongea mielekeo ya kushikamana na dini ya watu wa Azerbaijan na kusema kuwa: Kheri na maslahi ya serikali ya Azerbaijan imo katika kuwa pamoja na hisia za kidini za wananchi wake kwa kadiri kwamba, wananchi hawatakuwa na wasiwasi kutoka upande wa serikali kuhusu masuala ya kidini.
Ayatullah Khamenei amesema, uungaji mkono wa wananchi na kuwategemea wao ndiyo kinga kubwa zaidi mbele ya madola makubwa. Ameongeza kuwa, iwapo serikali ya Azerbaijan itaungwa mkono wa wananchi hakuna dola au nguvu yoyote inayoweza kuidhuru na sisi tunaiombea dua ya mafanikio serikali na taifa la Azerbaijan.
Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Rais Hassan Rouhani, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan ameashiria masuala ya kihistoria, kiutamaduni na kidini yanayozikutanisha pamoja nchi hizi mbili na kusema: Iran an Azerbaijan daima zimekuwa pamoja na kwamba safari ya karibu Waazerbaijani milioni moja nchini Iran mwaka uliopita ni kielelezo cha mfungamano huo wa kiutamaduni na kidini.   

 

700 /