Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran:

Dawa ya matatizo yaliyopo ni kutumia watumishi wenye uwezo

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Iran Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo amehutubia hadhara ya makamanda na maafisa wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya (saw) cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, kituo hicho ni mstari wa mbele wa kulinda heshima na nchi. Ameashiria mchango usio na mbadala wa watumishi katika maendeleo ya sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikosi vya jeshi na kusisitiza kuwa: Mnapaswa kustawisha vipawa vingi vya watumishi na kuvitumia katika kukidhi mahitaji na na kuondoa mapungufu ya nchi kwa kuchapa kazi na juhudi mtawalia.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, kutoa huduma katika mstari wa mbele wa kukabiliana na vitisho ni fursa yenye thamani kwa askari wenye ghera, waumini na sharifu wa Kituo cha Ulinzi wa Anga na kuongeza kuwa: Kazi nyingi nzuri zimefanyika katika kituo hiki na hii inaonesha azma, ari na uwezo wa askari wa kikosi hiki.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema watumishi na nguvukazi ya watu yenye elimu, tadbiri, ushujaa na isiyochoka ni msingi na nguzo imara ya kushinda na kuvuka vizuizi vyote.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, maendeleo mengi yaliyopatikana katika sekta na nyuga mbalimbali kama katika vikosi vya jeshi na vilevile katika uga wa elimu na teknolojia ni viashiria vya kuweko uwezo wa watumishi na nguvukazi ya vijana ya Iran yenye ari kubwa. Amesema watoto wenye uwezo wa Iran sawa wale wa ndani ya nchi au wale walioko katika vituo na taasisi za sayansi na teknolojia duniani ni fahari kubwa ya kujivunia.
Amesema kuwa, dawa ya kutibu baadhi ya matatizo yaliyopo nchini ni kutumia na kuhamasisha nguvu na vipawa hivyo. Amelipongeza jeshi la Iran katika Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khamuli Anbiya na ushirikiano wake na Wizara ya Ulinzi, vyuo vikuu na vituo vya elimu katika kukidhi mahitaji na kuondoa mapungufu yaliyopo na kusema kuwa: Endelezeni kazi na juhudi kwa bidii kubwa zaidi ya hapo awali na pigeni hatua kubwa mbele kwa kubuni mipango mipya kwa ajili ya kuifanya nchi ijitosheleze.
Kabla ya matamshi hayo ya Amiri Jeshi Mkuu, kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiya, Brigedia Jenerali Ismaili alitoa hotuba fupi kuhusu maadhimisho ya siku ya kuanzishwa kituo hicho na kutoa ripoti ya hatua zilizochukuliwa hadi sasa.  

 

700 /