Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Maadui wanafanya njama za kuzuia jihadi ya taifa la Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei adhuhuri ya leo amekutana na kufanya mazungumzo na familia ya Shahidi Muhsin Hojaji na kumtaja shahidi huyo kuwa ni msemaji wa mashahidi waliodhulumiwa na kukatwa vichwa. Ameashiria mahudhurio makubwa ya wananchi katika mazishi ya shahidi huyo na kusema: Mwenyezi Mungu SW amelipa izza na fahari taifa la Iran kupitia jihadi ya Muhsin azizi na amemfanya kuwa nembo ya kizazi cha vijana wa kimapinduzi na muujiza wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vilevile Ayatullah Khamenei ameashiria jinsi jina la Shahidi Hojaji lililovyopata umashuhuri mkubwa na kung'aa hapa nchini kutokana na jihadi na kuuliwa kwake shahidi na kusema kuwa: Mashahidi wote wamedhulumiwa na mbali na Shahidi Muhsin Hojaji, wako mashahidi wengine mbao adui aliwaua kwa kukata vichwa vyao na hao wote wana daraja za juu mbele ya Mwenyezi Mungu SW lakini Mwenyezi Mungu amemfanya (Shahidi Hojaji) kuwa mwakilishi na msemaji wa mashahidi hao wote kwa mujibu wa hekima na sifa makhsusi za kijana huyo.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mashahidi wote kutoka Iran, Afghanistan, Iraq na maeneo mengine waliouawa shahidi katika mapambano dhidi ya matakfiri waovu na vibaraka wa Marekani na Uingereza wamejumuika na kuonekana katika Shahidi Hojaji, na Mwenyezi Mungu amemfanya nembo ya mashahidi madhlumu na mashujaa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia jitihada kubwa zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kuliondoa taifa la Iran hususan vijana katika njia ya jihadi na kufa shahidi, kulifanya limsahau Imam Khomeini na kupotea njia ya wazi ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa: Kuvutiwa kwa nyoyo za vijana wengi kwenye masuala ya kimapinduzi katika mazingira kama haya ni jambo la kustaajabisha.
  Ayatullah Khamenei amesema kuwa, familia za mashahidi, viongozi na taifa lote la Iran lina deni kubwa kwa shahidi Hojaji na mfano wake. Amesifu nafasi na mchango mkubwa wa baba, mama na mke wa shahidi na kusema: Japokuwa kumpoteza shahidi ni msiba mkubwa kwa familia yake lakini izza na fahari ambayo Mwenyezi Mungu amelipa taifa kupitia shahidi huyo ni pozo na faraja kwa familia yake.
Ayatullah Khamenei ameandika maneno yafuatayo katika picha ya Shahidi Hojaji wakati aliposhikwa mateka na magaidi wa kundi la kiwahabi la Daesh: "Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya shahidi huyu aliyepata fahari kubwa ambaye alikuwa nembo ya haki inayopata ushindi mbele ya batili inayoangamia na kutoweka. Salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie yeye ambaye amepata izza na kulipa fahari taifa kutokana na mapambano yake ya jihadi yenye ikhasi na kuuliwa shahidi katika hali ya kudhulumiwa."
Muhsin Hojaji ambaye alikuwa miongozi wa vijana waliokwenda Iraq na Syria kulinda haram za watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) mbele ya hujuma za makundi ya kiwahabi na kitakfiri, aliuawa shahidi tarehe 9 Agosti mwaka huu baada ya kukamatwa mateka na kundi la kigaidi la Daesh katika mpaka wa Syria na Iraq.

700 /