Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Siri ya ushindi wa hivi karibu Iraq ni umoja na jihadi ya vijana

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo mapema leo katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi aliyeko safarini hapa mjini Tehran. Ameunga mkono hatua zilizochukuliwa na serikali ya Iraq kwa ajili ya kulinda mamlaka na ardhi yote ya nchi hiyo na kuitaja Iraq kuwa ni nchi muhimu katika ulimwengu wa Kiarabu.
Vilevile amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Iraq kwa ajili ya kupanua uhusiano na nchi jinari na za eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa: Sambamba na hayo, kuna ulazima wa kuwa macho na makini mbele ya hila za Wamarekani na kamwe msiwaamini.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Wamarekani ndio waliounda kundi la Daesh lakini sasa na baada ya kundi hilo kushindwa mbele ya serikali na wananchi wa Iraq, wanajifanya kuwa wako pamoja na Iraq katika tukio hilo muhimu; hata hivyo hapana shaka kuwa, wakati wowote watakapopata fursa watatoa tena pigo dhidi ya Iraq.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza suala la kuimarishwa zaidi uhusiano wa pande zote kati ya Tehran na Baghdad katika nyanja mbalimbali na akamwambia Bwana Haider al-Abadi kwamba: "Matafa mbalimbali ya kanda hii yanayapa mazingatio mafanikio ya Iraq kutokana na jitihada kubwa na ushujaa wa watu wa Iraq, wewe mwenyewe na viongozi wengine wa Iraq".
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Iraq ameashiria jitihada zinazofanywa na wananchi na vijana wa Iraq kwa ajili ya kulinda umoja na ardhi yote ya nchi hiyo na kusema: Tunalinda umoja na ardhi yote ya Iraq kwa uangalifu kamili, na kama tulivyowaambia ndugu zetu wa Kurdistan, hatutaruhusu hatari ya kujitenga itishie nchi yetu.
Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Is'haq Jahangiri, Bwana Haider al-Abadi ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na himaya na misaada yake kwa Iraq katika mapambano yake dhidi ya magaidi na kusema: Tunafanya jitihada kubwa kwa ajili ya kupanua zaidi uhusianio na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.       

 

700 /