Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ayatullah Khamenei:

Nina imani vijana waumini watajenga vijiji bora zaidi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kukagua maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi katika mkoani Kermanshah huko kaskazini magharibi mwa Iran kwa kutembelea vijiji vya Kuik Majiid, Kuik Aziz, Kuik Hassan, Sarab Zahab na Qal'eye Bahadori. 
Akiwa pamoja na wananchi wa vijiji hivyo, Ayatullah Khamenei ameeleza mshikamano wake na watu waliopatwa na msiba wa maeneo hayo na kuongeza kuwa: Tangu saa za mwanzoni baada ya tetemeko la ardhi niliwaagiza maafisa wa nchi kushughulikia wananchi ili baadhi ya matatizo yenu yatatuliwe na kwa bahati nzuri vikosi vya Jeshi la Taifa na taasisi za kiraia vimefanya kazi nzuri hadi hivi sasa na kuna ulazima wa kudumishwa juhudi hizo. 
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria hasara kubwa iliyosababishwa na tetemeko la ardhi la siku kadhaa zilizopita na kuharibiwa kikamilifu baadhi ya vijiji na kusema: Nimefurahi sana kukutana kwa karibu na nyinyi vijana waumini na watanashati na nina imani kwamba, kwa rehma zake Mwenyezi Mungu, jitihada za maafisa wa nchi, hima ya wananchi na nyinyi vijana wapendwa, vitajengwa vijiji bora zaidi ya hapo kabla. 
Vilevile amemuomba Mwenyezi Mungu Muweza kuwapa subira, sakina na rehma zake wanawake na wanaume wenye ghera na waaminifu wa Kermanshah na kusema: Hii leo tunashirikiana na nyinyi katika ghamu na masaibu haya na tunatarajia kwamba, tutaweza kujenga maisha mapya ili tuweze kushirikiana na nyinyi pia katika nyakati za furaha. Amesema anatajia tukio hilo litakuwa sababu ya kupunguzwa machungu ya vijiji vya Kermanshah ambavyo kabla ya mtetemeko wa ardhi pia vilikuwa vikisumbuliwa na matatizo mengi. 
Kikao cha kushughulikia matatizo ya watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi na kuchukua maamuzi kuhusu ujenzi mpya na operesheni za misaada kwa watu wa eneo hilo pia kimefanyika kikihudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na maafisa husika.         
 

700 /