Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Kuna ulazima wa kudhaminiwa makazi kwa waathirika wa zilzala

Baada ya kukagua maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amehutubia kikao cha kushughulikia matatizo ya waathiriwa wa tetemeko hilo kilishoshirikisha maafisa wa kimkoa, viongozi wa kieneo na baadhi ya makamanda wa jeshi na polisi akisema kuwa, viongozi hao wana majukumu mazito ya kushughulikia watu waliopatwa na masaibu ya tetemeko hilo la ardhi mkoani Kermanshah. 
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, suala linalopaswa kupewa kipaumbele katika hali ya sasa ni kudhamini makazi kwa watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi na kujenga upya maeneo yaliyoharibiwa au kupatwa na madhara. Amesisitiza kuwa kazi hiyo inapaswa kufanyika haraka kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali za kijeshi na kiraia na kwa usimamizi mmoja na wa kijihadi. 
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi wanapaswa kuhisi maendeleo ya kazi zilizofanyika na kuongeza kuwa, maeneo mengi yameharibiwa katika mtetemeko wa ardhi na ingawaje mji wa Sarpol-e-Zahab na baadhi ya maeneo mengine yamepata hasara kubwa, lakini baadhi ya vijiji vimeharibiwa kabisa, jambo ambalo linapaswa kupewa umuhimu. 
Ameashiria masaibu, mashaka na matatizo ya watu waliopatwa na tetemeko hilo la ardhi na kusema: Kwa kuwa sisi hatujakumbwa na tetemeko la ardhi yumkini tusielewe vyema masaibu na mashaka ya watu waliokumbwa na janga hili. "Watu ambao hadi juzi tu walikuwa pamoja na familia zao katika nyumba moja wakiishi kwa amani na utulivu, wamepoteza maisha yao mara moja, na sasa katika kipindi hiki cha baridi kali maisha yao yameishia katika mahema", amesisitiza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. 
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kutambua umuhimu wa tukio hilo ili tupate kutambua umuhimu wa majukumu yetu na kuongeza kuwa: Wakati wa matukio kama zilzala, miongoni mwa mambo ya muhimu zaidi katika nyakati za mwanzoni mwa kutokea kwake ni suala la uokoaji ambalo kutokana na kufika haraka vikosi vya jeshi na polisi katika eneo hili limefanyika kwa njia inayokubalika.
Amesema kuwa, kufuatia ukaguzi alioufanya kwenye baadhi ya maeneo yaliyopatwa na tetemeko la ardhi na ukubwa wake, inabainika kuwa lau kama suala la uokoaji lisingefanyika haraka na mapema basi hapana shaka kuwa hasara ingekuwa kubwa mara kadhaa ya ile iliyotokea.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria vikao vyake na maafisa wa serikali wakati wa tetemeko la ardhi la Bam hapa nchini (miaka kadhaa iliyopita) na kusema: Kufuatia vikao hivyo kuliundwa Tume ya Kusimamia Majanga na Migogoro ambayo itakuwa inachukua hatua za haraka na mapema za kushughulikia majanga ya kimaumbile.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa suala la "kutoa misaada" baada ya operesheni za "uokoaji" ni miongoni mwa mambo muhimu katika matukio na majanga ya kimaumbile na kusisitiza kuwa: Japokuwa kasi inahitajika pia wakati wa kutoa misaada lakini operesheni za misaada si suala la papo na hapo na linaloisha na kumalizika, kwa sababu lina vitengo vyake wakati na zama zote.
Amesema katika matukio kama zilzala, kudhaminiwa masuala kama chakula, maji, suhula za awali za maisha na mavazi vinapaswa kupewa mazingatio katika awamu za kwanza za uokoaji, lakini baada ya awamu hizo suala muhimu zaidi huwa ni kukusanya takataka mijini na vijijini na kisha kutayarisha makazi na nyumba kwa ajili ya waathiriwa, kazi ambayo ni kubwa na ngumu lakini lazima ifanyike.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kasi katika kujenga nyumba za wananchi zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi na kudhamini vifaa vya joto (kwa ajili ya msimu wa baridi) ni miongoni wma mabo muhimu sana na ya dharura na kuongeza kuwa, ili kutekelezsa majukumu hayo mazito kuna ulazima wa kuwepo usimamizi mkuu unaojumuisha tasisi zote (centralized management).
Ayatullah Khamenei ameshukuru juhudi kubwa zinazofanywa na maafisa wa nchi hususan jumuiya na taasisi zilizofanya hima kubwa kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi na zilizoanza kazi mara moja baada tu ya tukio hilo. Amesema mbali na kuweko usimami mmoja (Centralized management) viongozi wa nchi pia wanapaswa kufanya kazi za kijihadi na kwa kasi na kufuatilia kazi zinavyoendelea.        
      
 

700 /