Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu:

Sharti la mafanikio ni kuunganisha sayansi za jamii na dini

Katika hotuba hiyo Ayatullah Khamenei alisema kuwa ni jambo la dharura kurejea kwenye Qur'ani tukufu na kupata jibu la masuala mbalimbali ya kifikra, kielimu, kisiasa na kijamii yakiwemo masuala muhimu ya sayansi za jamii. Amesisitiza kuwa, katika baadhi ya matawi ya sayansi za jamii kumefanyika utafiti na ukosoaji kwa zaidi ya mamia kadhaa ya miaka duniani na utangulizi wa kuingia katika sayansi za jamii na kuitenganisha na asili na misingi isiyo ya kidini au inayopingana na dini na kisha kuiunganisha ya Qur'ani na ufunuo (wahyi) ni kujua vyema na kikamilifu kazi na maendeleo yaliyopatikana duniani katika uwanja huo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo udharura wa kufanyika utafiti na uhakiki katika sura ya kazi za kimakundi na vilevile udharura wa kushirikiana na vituo na makundi mbalimbali ambayo yanafanya uhakiki na kazi ya kuelekeza sayansi za jamii upande wa mafundisho ya Kiislamu na kusema: Mbali na wahakiki wa ndani ya nchi, baadhi ya wanafikra katika ulimwengu wa Kiislamu pia wanafanya utafiti na uhakiki katika masuala ya sayansi za jamii za Kiislamu; hivyo kuna ulazima kwa taasisi kama Chuo Kikuu cha al Mustafa kuwaarifisha watu hao na kazi zao na kutayarisha uwanja wa kuwepo ushirikiano na mshikamano katika upeo mpana zaidi wa kimataifa. 
Ayatullah Khamenei amesisitiza ulazima wa kuzidishwa ubora wa tafiti za kisayansi na kielimu na kueleza matarajio ya kuzalishwa makala zenye ufumbuzi na za kina katika Kongamano la Kimataifa la Qur'ani na Sayansi za Jamii. Amesema baadhi ya athari na kazi zilizoandikwa na wasomi vijana na wenye fikra mpya wa Qum zina thamani kubwa, zinatia matumaini na kutoa bishara ya kuanza harakati kubwa zaidi na inayosonga mbele ya uhakiki na utafiti katika vyuo vikuu vya kidini.

700 /