Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran:

Kuimarishwa vikosi vya jeshi kunalinda taifa

Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia uhasama usiokoma wa maadui dhidi ya taifa la Iran na Mfumo wa Kiislamu hapa nchini na kusema kuwa, kukabiliana na mahasimu hao kunahitajia kuimarishwa zaidi uwezo wa jeshi la taifa.
Ayatullah Ali Khamenei ameyasema hayo adhuhuri ya leo katika hadhara ya makamanda wa ngazi za juu wa vikosi vya Jeshi la Taifa na washindi wa Tamasha la Malik Ashtar waliokwenda kuonana naye na kusisitiza kuwa, Jeshi la Taifa la Iran linahitajia watumishi bora zaidi katika upande wa kifikra, kivitendo, azma na irada ili waweze kulilinda taifa mbele ya maadui. 
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kufurahishwa kwake na hatua ya kuimarishwa harakati inayosonga mbele zaidi ya majeshi ya Iran katika upande wa watumishi na kuongeza kuwa, sharti la kupiga hatua kubwa zaidi katika mafanikio ni kudumishwa harakati inayoendelea mbele bila ya kusita; hivyo kuna ulazima wa kila sekta kuchapa kazi zaidi katika majukumu yake.
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Iran amesema kuwa, tamasha hilo kupewa jina la Malik Ashtar ambaye alikuwa mmoja kati ya makamanda na masahaba wa Amirul Muumunin Ali bin Abi Twalib (as) kunatoa mafunzo na darsa na kusisitiza kuwa: Malik Ashtar alikuwa mtu adhimu na kigezo cha kuigwa katika kuona mbali na kutambua njia iliyonyooka, azma kubwa, katika kuwajibika na kuwa tayari kwa ajili ya jihadi, ushujaa na katika ukamanda na wakati huo alikuwa ruwaza njema katika masuala ya kiroho, ibada, uchamungu na unyenyekevu. Amesisitiza kuwa makamanda wa vikosi vya jeshi la Iran wanapaswa kuimarisha masuala hayo ya kiroho katika nafsi zao kabla ya watu wengine.   
kabla ya hotuba ya Amiri Jesh Mkuu, kamanda wa majeshi ya Iran, Meja Jenerali Baqiri ametoa mkono wa pongezi kutokana na ushindi mkubwa na wa kistratijia wa kambi ya muqawama na mapambano na kusema kuwa, makamanda 52 na maafisa wengine wa ngazi juu wa jeshi wameshinda na kuenziwa katika Tamasha la 8 la Malik Ashtar. 
 

700 /