Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Moyo ya kishujaa, kujitolea na imani ni kinga mbele ya maadui

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu adhuhuri ya leo amekutana na baadhi ya familia za mashahidi watukufu na kusema kuwa heshima, usalama na maendeleo ya Iran yametokana na kujitolea na kujitoa mhanga kwa mashahidi.
Ayatullah Khamenei amezungumzia matukio ya hivi karibuni na njama za maadui wanaotaka kutoa pigo kwa Mfumo wa Kiislamu wa Iran na kusema: "kile ambacho kimemzuia adui kutekeleza uadui wake ni kuwepo moyo wa kishujaa, kujitolea na imani katika taifa."
Ayatullah Khamenei ameashiria ukweli kuwa, adui anasubiri fursa na mwanya wa kujipenyeza na kutoa pigo kwa taifa la Iran na kuongeza kuwa, katika matukio ya hivi karibuni, maadui wa Iran wakitumia mbinu na zana mbalimbali walizonazo kama vile pesa, silaha, siasa na mashirika yao ya usalama wameungana kwa ajili ya kuzusha matatizo katika Mfumo wa Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kuhusiana na mazingira yaliyopo, ana kauli ambayo atawabainishia wananchi wa Iran kwa wakati wake.
Ayatullah Khamenei pia amezungumzia nafasi muhimu ya moyo ya kishujaa na kujitolea katika kumzuia adui kutekeleza uhasama wake na kusema: "Mashahidi ni mfano kamili wa moyo huu na jihadi katikka njia ya Mwenyezi Mungu. Ameongeza kuwa, taifa la Iran daima lina deni kwa mashahidi azizi ambao waliacha nyumba na familia zao na kwenda kukabiliana na adui khabithi ambaye alikuwa anapata uungaji mkono wa kambi za Mashariki na Magahribi na madola yapingayo mapinduzi na ustawi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria hali ya kusikitisha ya baadhi ya nchi za eneo la Asia Magharibi na Afrika Kaskazini na kukumbusha kuwa: "Iwapo wakati wa vita vya kulazimishwa adui Mbaathi (utawala wa Saddam) angeweza kuingia Iran basi hangehurumia chochote na hali ya Iran ingekuwa mbaya zaidi ya ile inayoshuhudiwa huko Libya na Syria hii leo."
Amezipongeza familia za mashahidi na kusema kuwa, thamani ya baba na mama wa mashahidi na ushujaa na kujitolea kwao si kazi ndogo kuliko kazi iliyofanywa na vijana wao waliouliwa shahidi, na watu hawa wana haki kubwa kwa taifa na nchi hii. 

700 /