Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Fikisheni ujumbe wa kisiasa wa Hija kwa Waisla

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu adhuhuri ya leo amekutana na kuzungumza na maafisa wanaosimamia ibada ya Hija wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 
Ayatullah Ali Khamenei amesema katika hadhara hiyo kwamba, amri ya Mwenyezi Mungu inayowataka Waislamu (wenye uwezo) kukusanyika sehemu moja maalumu na wakati mmoja kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija inabeba jumbe nyingi muhimu za kisiasa kama ulazima wa kuwepo mawasiliano na ushirikiano baina ya Waislamu na kuonesha nguvu ya Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Mbali na upande wa masuala ya kiroho wa Hija ambayo yana umuhimu mkubwa, hakika na malengo hayo ya Kiislamu pia yanapaswa kudhihirishwa na kuwekea mipango na ratiba.
Ayatullah Khamenei amesema, kuwasiliana na Waislamu wakati wa ibada ya Hija, kufikisha ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mahujaji na kujibu maswali na shubha zao, kutayarisha uwanja mzuri wa kuanzishwa au kuimarishwa mahusiano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine za Waislamu na kuishi pamoja kiudugu makundi mbalimbali ya Waislamu ni miongoni mwa jumbe za kisiasa na za dharura kwa ajili ya Ulimwengu wa Kiislamu katika siku za Hija. Amesisitiza kuwa, upande wa kisiasa wa Hija haupaswi kusahauliwa na Hija ya Nabii Ibrahim ambayo imehuishwa tena baada ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran inatofautiana na Hija ya kabla yake na Hija ya nchi ambazo hajiwahi hata kunusa harufu ya misingi ya Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria vizuizi vinavyowekwa na serikali ya Saudi Arabia dhidi ya vikao vya kusoma dua ya Kumeil wakati wa ibada ya Hija na akasema: Kuna ulazima wa kufanya jitihada na kubuni njia za kuvuka vizuizi na hasara hiyo.
Ayatullah Ali Khamenei pia amekosoa vikali mwenendo wa serikali ya Saudi Arabia wa kuharibu na uvunjaji wake mkubwa wa turathi za Kiislamu kama zile zinazohusishwa na Mtume Muhammad (saw), Amirul Muuminin Ali bin Abi Twalib (as), makhalifa na wapiganaji jihadi wa zama za awali za Uislamu kwa kisingizio cha kupanua maeneo ya ibada ya Hija na kusema: Wakati nchi mbalimbali zinahifadhi na kulinda kwa makini athari zao za kihistoria na wakati mwingine zinabuni athari bandia kwa ajili ya kukuza matunda ya historia yao, athari nyingi za kale za Kiislamu Makka na Madina zimeharibiwa hadi hivi sasa. 
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jumuiya ya Hija na Ziara ya Iran na taasisi nyingine husika zinawajibika kuchukua hatua, kubuni mbinu na kuwasiliana na maafisa wa Hija wa nchi nyingine za Kiislamu kwa ajili ya kuzuia kuharibiwa mabaki ya turathi za Kiislamu (huko Saudi Arabia).    
Vilevile amewataka maafisa wa Hija wa Iran kutumia zana za kisasa hususan mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwasiliana na mahujaji wa nchi nyingine katika siku za ibada ya Hija na kuzidisha ushirikiano. 
 

700 /