Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika Kongamano la Kimataifa la Palestina

Amesema, miongoni mwa matukio muhimu yaliyotokea katika kipindi cha baina ya kikao cha leo na kikao cha kabla yake yaani cha tarehe 15 hadi 17 Mfunguo Sita - Rabiul Awwal 1427 Hijria kilichofanyika pia mjini Tehran ni kufeli na kushindwa kimaajabu Israel katika upande wa kijeshi na kisiasa mbele ya Istikama ya Kiislamu kwenye vita vya siku 33 vya Lebanon mwaka 1427 Hijria na kufeli kifedheha utawala wa Kizayuni katika jinai zake kwenye vita vya siku 22 dhidi ya wananchi na serikali halali ya Palestina huko Ghaza.

Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa utawala ghasibu wa Israel kwa makumi ya miaka ulikuwa unatumia jeshi na silaha zake huku ukiungwa mkono kijeshi na kisiasa na Marekani kuonyesha kuwa una nguvu za kutisha zisizoshindika. Lakini kwa mara nyingine vikosi vya wanamapambano wa Kiislamu vinavyoendesha mapambano yake kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na uungaji mkono wa wananchi kuliko kutegemea silaha na zana za kijeshi vimefanikiwa kuishinda tena Israel. Licha ya utawala huo kufanya mazoezi mbalimbali na kujiandaa vilivyo kijeshi na kwa kutegemea mashirika makubwa ya kijasusi na uungaji mkono usio na kikomo wa Marekani na baadhi ya tawala za Magharibi zikishirikiana na baadhi ya wanafiki katika ulimwengu wa Kiislamu, hivi sasa umejikuta ukielekea kuporomoka vibaya na ukiwa dhaifu sana mbele ya wimbi kali la mwamko wa Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kwamba, kuua idadi kubwa ya raia, kuharibu nyumba zisizo na ulinzi, kutoboa kwa risasi vifua vya watoto wachanga, kushambulia mashule na misikiti kutumia mabomu ya fosforasi na baadhi ya silaha nyingine zilizopigwa marufuku, kufunga njia za kuingizwa chakula, madawa, mafuta na mahitaji mengine ya lazima ya wananchi wa Ghaza kwa muda unaokaribia miaka miwili na jinai nyingine nyingi ni mambo yanayothibitisha kuwa siasa zile zile na mtindo ule ule wa maisha ya kikatili yasiyo na huruma uliotumiwa katika maafa ya Diryasin, Sabra na Shatila bado uko vile vile leo hii katika fikra na nyoyo za kidhumla za mataghuti hawa wa zama hizi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapindizi ya Kiislamu ameongeza kuwa, licha ya kuweko juhudi kubwa za kishetani na za kutisha kwa kiasi chote hicho lakini maghasibu na waungaji mkono wao si tu wameshindwa kuupa uhalali utawala wa Kizayuni lakini pia suala la kuwepo Israel limekuwa tata zaidi ikilinganishwa na huko nyuma.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, kushindwa kuwa na stahamala vyombo vya habari vya Magharibi na Kizayuni pamoja na tawala zinazounga mkono Uzayuni mbele ya hata kuulizwa swali na kufanyika utafiti tu kuhusu ngano ya Holocaust ambayo ndiyo iliyotumika kuikalia kwa mabavu Palestina, ni moja ya dalili za kuweko utata na kuchanganyikiwa huko.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, hivi sasa na kuliko wakati mwingine wowote uliopita, hali ya utawala wa Kizayuni imezidi kuwa mbaya ndani ya fikra za walimwengu na udadisi kuhusu sababu za kuundwa utawala huo unazidi kupata nguvu.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa upinzani ambao haujawahi kushuhudiwa mfano wake uliolipuka wenyewe ulimwenguni kuanzia mashariki mwa Asia hadi Amerika ya Latini dhidi ya utawala wa Kizayuni na maandamano ya wananchi katika nchi 120 duniani zikiwemo za Ulaya na Uingereza ambayo ndiyo mwasisi mkuu wa mti huo khabithi (utawala wa Kizayuni wa Israel) sambamba na uungaji mkono wa walimwengu kwa Istikama ya Kiislamu ya Ghaza na Istikama ya Kiislamu ya Lebanon katika vita vya siku 33 ni vitu vinavyoonyesha kuwa dunia imeanza kushuhudia mapambano ya kimataifa dhidi ya Uzayuni na kwamba haijawahi kushuhudiwa mapambano kama hayo katika kipindi cha miaka 60 ya tangu kuasisiwa Israel si katika upande wa kiwango, wala ukubwa na wala uzito wake.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, kosa kubwa linalofanywa kuhusu kadhia ya Palestina na ambalo limepandikizwa katika fikra za baadhi ya watu ni kule kudai kuwa njia pekee ya kuweza kuokoka taifa la Palestina ni kufanya mazungumzo.

Ayatullah Udhma Khamenei amesema, hata Rais mpya wa Marekani ambaye ameingia madarakani kwa kaulimbiu ya mabadiliko katika siasa za serikali ya Bush anapiga domo la kushikamana bila masharti na suala la kudhamini usalama wa Israel yaani kulinda ugaidi wa kiserikali, kutetea dhulma na ubeberu, na kutetea mauaji ya umati ya mamia ya wanaume, wanawake na watoto wadogo wa Palestina; hiyo kwa kweli ni kuendeleza upotofu ule ule wa kipindi cha Bush na si kitu kingine.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, njia ya kuweza kuokoka Palestina ni istikama na kusimama kidete tu na kusisitizia haja ya kuweko mshikamano na kuwa kitu kimoja taifa la Palestina.

Vile vile amesema, kuwasaidika kikamilifu na kwa kila njia waanchi wa Palestina pamoja na kuwaunga mkono kikamilifu wananchi hao madhlumu ni "wajibu kifaya" kwa Waislamu wote na kuongeza kuwa, zile tawala ambazo zinailaumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na baadhi ya nchi nyingine za Kiislamu kwa kuwasaidia Wapalestina nazibebe jukumu hilo na ziliunge mkono taifa la Palestina ili kuwaondolea wengine wajibu na jukumu hilo la Kiislamu, lakini kama hazina hima, wala uwezo na wala ushujaa wa kufanya hivyo, ni vyema kwao badala ya kulaumu na kukwamisha mambo washukuru hatua za kutekeleza wajibu na za kishujaa zinazochukuliwa na wengine.

Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amesema ujenzi mpya wa Ghaza ni miongoni mwa masuala yanayopasa kutekelezwa kwa haraka sana na kwamba Hamas ambayo imechaguliwa kwa kura mutlaki na Wapalestina pamoja na hamasa na istikama yake iliyoukwamisha utawala wa Kizayuni ni nukta inayong'ara zaidi katika historia ya miaka 100 iliyopita ya Palestina. Amesema inabidi Hamas kuwa kitovu cha kazi zote zinazohusiana na ujenzi mpya wa Ghaza.

700 /