Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Mwaka mpya ninauita mwaka wa Marekebisho ya Kigezo cha Matumizi katika Nyanja na Mambo Yote

Ayatullah Khamenei amesema kuwa kukaribiana kwa sikukuu ya Nairuzi ya mwaka huu na siku za maulidi na kuzaliwa Mtume wa Mwisho Muhammad (saw) na Imam Ja'far Swadiq (as) kumeipa baraka zaidi sikukuu hiyo na amewapa mkono wa idi wananchi wa Iran, wageni kutoka nje ya nchi na mataifa yote yanayosherehekea sikukuu hii na akawatakia wote mwaka uliojaa mema na ufanisi. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka uliopita wa 1387 kuwa ulijaa matukio mengi. Ameashiria matukio muhimu ya ndani ya nje ya mwaka huo na akasema: Mwaka 1387 ulianza kwa habari nzuri za nyuklia ambazo zilithibitisha uwezo wa taifa la Iran na wasomi waliotabahari wa nchi hii, na kwamba kurushwa angani satalaiti ya Omid (Matumaini) kumeiweka Iran katika orodha ya nchi kadhaa duniani zenye teknolojia hiyo muhimu. Amesisitiza kuwa maendeleo hayo ambayo kwa hakika ni ya kustaajabisha, yamelipa taifa la Iran hadhi na itibari mpya.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria pia kuzinduliwa kwa muda na kwa ajili ya majaribio kinu cha nyuklia cha Bushehr huko kusini mwa Iran na akasema: Dunia imeamini kwamba njia ya maendeleo ya nyuklia ya Iran haiwezi kufungwa kwa sababu ustawi na maendeleo ya Iran katika nyanja mbalimbali za kielimu na kadhalika ni dalili ya kufeli vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa hili. Amesema kuwa maendeleo hayo yanathibitisha kwamba taifa kubwa la Iran linafanya harakati na kustawi na linazima propaganda na njama za maadui wake kwa kutegemea vijana wake wenyewe hima na fahari kubwa.

Katika ujumbe huo wa sikukuu ya Nairuzi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu vilevile ameashiria kuundwa Bunge la Nane la Iran na kazi nzuri zilizofanywa kwa ushirikiano wa Bunge hilo la Serikali na akasema kuwa, anatarajia ushirikiano huo utaendelea.

Katika medani ya masuala ya uchumi amezungumzia mgogoro mkubwa wa kiuchumi duniani na akasema: Licha ya mgogoro huo mkubwa ulioanzia Marekani na kuzusha tufani shadidi ulimwenguni, na licha ya vikwazo mbalimbaliu dhidi ya Iran, viongozi wa nchi hii wamefanikiwa kuilinda nchi na taifa mbele ya wimbi kubwa la matatizo yaliyosababishwa na mgogoro wa kimataifa. Amesisitiza kwamba zinapaswa kuchukuliwa tahadhari na kufanyika juhudi zaidi ili maendeleo ya kiuchumi yachanue na kunawiri zaidi.

Ayatullah Khamenei ameeleza kuridhishwa na "ubunifu na maendeleo" yaliyopatikana katika mwaka uliomalizika wa 87 Hijria Shamsia na akasema kwamba, kazi zilizofanyika mwanzoni mwa utekelezaji wa kaulimbiu hiyo ni nzuri lakini kaulimbiu ya "Ubunifu na Kuchanua" inabidi iendelee kutekelezwa kwa nguvu zote ili taifa la Iran lifikie kiwamgo lilachostahiki.

Ayatullah Ali Khamenei ameashiria masuala muhimu yaliyotokea katika mwaka 87 Hijria Samsia kama mgogoro wa kiuchumi duniani, mashambulizi yaliyofeli ya siku 22 ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na mapambano yanayostahiki pongezi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina na akasisitiza kuwa, kushindwa kwa fedheha kwa Wazayuni kumewapa walimwengu tajiriba muhimu mno kwamba wanaweza kusimama kidete mbele ya madhalimu na kuwashinda.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya wa 1388 Hijria Shamsia kuwa ni mwaka muhimu, na huku akiashiria dua ilinayosomwa wakati wa kuingia mwaka mpya amesema: Kubadilishwa hali ya taifa la Iran na kuwa hali bora zaidi kunahitaji taufiki na rehema ya Mwenyezi Mungu lakini inatupasa kuelewa kwamba taufiki na reheme na Mwenyezi Mungu inategemea jihudi na hima ya wananchi wote ili kuleta mabadiliko katika maisha ya mtu binafsi na jamii.

Akifafanua nyanja zinazohitajia mabadiliko na marekebisho, Ayatullah Khamenei ameashiria suala la "israfu na ubadhirifu wa mtu binafsi na umma" na utumiaji ovyo wa rasilimali mbalimbali za nchi na akasema kuwa, Uislamu Mtukufu na watu wenye akili na busara duniani wanasisitiza kwamba utumiaji wa mali unapaswa kufanyika kwa tadbiri na busara.

Mwishoni mwa ujumbe wake wa sikukuu ya Nairuzi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba" Sisi sote hususan viongozi wa Vyombo Vitatu Vikuu vya Utawala, shakhsia wa kijamii na wananchi wote, tunapaswa kuweka ratiba ya kutekeleza kaulimbiu hiyo muhimu na ya kimsingi ya "Marekebisho ya Kigezo cha Matumizi  katika Nyanja Zote" na kupiga hatua katika njia hiyo katika mwaka huu mpya ili kielelezo cha kubadilisha hali ya taifa na kuifanya hali bora na nzuri zaidi kiweze kudhihiri kwa kutumia kwa busara na kwa njia sahihi rasilimali za nchi.  

        

700 /