Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa kufariki dunia Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Abdul Aziz al Hakim

Huduna kubwa za mwanazuoni huyu katika kuunda serikali ya kitaifa ya Iraq kamwe hazitasahaulika

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe akieleza kusikitishwa na kifo cha Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Abdul Aziz al Hakim aliyeaga dunia jana mjini Tehran. Matini ya ujembe huo inasema:

Bismillahir Rahmanir Rahim

Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari ya kuaga dunia na kurejea kwa Mola Mwenyekiti wa Majlisi Kuu ya Kiislamu ya Iraq Hujjatul Islam Sayyid Abdul Aziz al Hakim.

Kifo hicho ni msiba mkubwa kwa taifa na serikali ya Iraq, na ni tukio la kuumiza mno kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sayyid Abdul Aziz alikuwa mtoto wa mwisho kati ya wana wa marjaa na kiongozi mkubwa wa kidini wa Waislamu wa Shia marehemu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Muhsin al Hakim ambao wote walipata daraja ya juu ya kuuawa shahidi katika njia ya kupambana na utawala wa umwagaji damu wa chama cha Baath huko Iraq na vibaraka wa ubeberu au walikabiliwa na mitihani migumu katika jihadi hiyo.

Huduna kubwa za mwanazuoni huyo mpiganaji wa jihadi katika njia ya kuunda serikali ya kitaifa ya Iraq tangu alipokuwa nchini Iran hadi baada ya kuondolewa madarakani serikali ya Saddam Hussein na kurejea nchini kwake, hazina kifani na kamwe hazitasahaulika.

Nimesikitishwa mno na tukio hilo na ninatuma salamu za rambirambi kwa ndugu zetu wa Iraq, serikali na Baraza Kuu la Kiislamu la Iraq na familia kubwa ya Hakim hususan wanaye na hasa Sayyid Ammar al Hakim.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu ampe maghufira na rehema zake. Vilevile ninamuomba Mwenyezi Mungu alipe maendeleo na ustawi taifa na serikali ya Iraq.

Sayyid Ali Khamenei

05/Shahrivar/1388, sawa na tarehe 6 Ramadhani 1430 Hijria  

700 /