Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu Asema katika Ujumbe wa Siku ya Kuwaenzi Mashahidi:

Mashahidi ni Dhihirisho la Kipindi Chenye Thamani Kubwa cha Kujilinda Kutakatifu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe kwa mnasaba wa siku ya kuadhimisha na kuwaenzi mashahidi na wale waliojitolea katika kipindi cha miaka 8 ya kujilinda kutakatifu akisema kuwa mashahidi ni dhihirisho na vinara wa kipindi hicho cha thamani kubwa. Ayatullah Khamenei amesema kuwa kuwaenzi mashahidi azizi na wenye daraja ya juu ambao walidhihirisha johari inayong'ara ya taifa lenye imani la Iran kwa kusabilia nafsi zao, kunaleta uhai mpya.

Matini ya ujumbe huo ambao umesomwa na mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika Taasisi ya Shahidi, Muhammad Hassan Rahimian wakati wa kusafisha makaburi ya mashahidi katika eneo la Behest Zahra, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehma, Mwenye kurehemu

Hamasa ya taifa la Iran katika kipindi cha kujilinda kutakatifu imeonyesha kilele cha uwezo wa kibinadamu wa watu wa ardhi hii ya Mwenyezi Mungu. Uwezo wa kusimama kidete na ushujaa, uwezo wa uvumbuzi na ubunifu, uhodari wa kiwango cha juu, mahusiano ya kifikra na kiroho, usafi na utakasifu wa nafsi na fikra za Kiirani, na zaidi ya yote, imani kubwa yenye taathira na inayoleta mabadiliko ya taifa hili linalompwekesha Mwenyezi Mungu, ilidhihirishwa katika kombe la dunia la kipindi hicho kilichokuwa na matukio mengi. Dhihirisho na vinara wa kipindi hicho chenye thamani kubwa ni mashahidi azizi na wenye nafasi za juu ambao waliimarisha jengo hili na kudhihirisha johari inayong'ara ya taifa la waumini kwa kutoa mhanga nafasi zao.

Kuwakumbuka mashahidi hao kunatoa uhai kwa taifa la Iran mithili ya kutia damu mwilini. Kuwaenzi na kuwakumbuka huku kunapasa kubakishwa hai siku zote.

Salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na jamaa zao wenye subira waliobakia hai na salamu za Mola ziwe juu ya wale wote wanaojitolea katika njia ya haki.

Sayyid Ali Khamenei

 

700 /