Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu katika Mkutano wa 18 wa Taifa wa Swala:

Ijazeni Miskiti kwa Harakati na Nishati Kama Zilivyo Nyoyo za Vijana

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei amesema katika ujumbe wake uliosomwa kwenye Mkutano wa 18 wa Taifa wa Swala kwamba kuupa mkutano wa mwaka huu jina la vijana ni hatua inayostahili pongezi. Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa kuwaelimisha vijana kuhusu usafi na raha ya Swala ni huduma kubwa mno kwao na kwa mustakbali utakaojengwa kwa hima ya vijana hao.

Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Kuuita mkutano wa mwaka huu wa Swala kwa jila la vijana ni hatua nzuri inayotokana na mtazamo sahihi kwa chemchemi hiyo inayotiririka ya kuomba na kumtaradhia Mola Mlezi. Moyo ambao haujachafuka wa kijana ndiyo kituo kilichotayari zaidi ambao taa hii yenye nuru na mahudhurio yake vinaweza kueneza joto na mwanga ndani yake na kudhihirisha njia ya safari ya kimaanawi kati ya njia nyingi za upotofu. Kuwaelimisha vijana usafi na raha iliyomo ndani ya ibada ya Swala na kumtaja Mwenyezi Mungu ni huduma kubwa kwa kizazi hicho na mustakbali unaopasa kujengwa kwa mikono na azma yao wenyewe.

Ninawausia kuisafisha misikiti, kuipamba na kuijaza kwa harakati, nishati na uhai kama zilivyo nyoyo za vijana. Misikiti inapasa kuwa vituo ambako taa ya Swala inawaka ndani yake na nuru ya maarifa, upendo na usafi wa moyo unang'ara ndani.

Maimamu wa Swala za jamaa, kamati za misiki na wahudumu wake kila mmoja wao anapasa kutekeleza sehemu ya wajibu huo mkubwa na wenye taathira.

Ninawatakia taufiki ya Mwenyezi Mungu wahusika wote wa mikutano ya Swala hususan Hujjatul Islam Muhsin Qaraati, rijali mstahiki na mwenye misimamo imara.

Sayyid Ali Khamenei

12 Aban 1388

03 Novemba 2009  

700 /