Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu

Kipindi cha Uongozi wa Bwana Zarghami Chaongezwa kwa Miaka Mingine Mitano

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza muda wa kuhudumu Sayyid Ezzatollah Zarghami kama Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRIB. Katika ujumbe wake uliotolewa Jumamosi, Ayatullahil Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya kutumiwa mafanikio ya sasa ya shirika la IRIB na hima kubwa kwa ajili ya kuondoa nakisi na mapungufu yaliyopo na kukifikisha chombo hicho cha kiutamaduni katika daraja ya chombo cha habari ambacho dini maadili mema, matumaini na kuelimisha jamii vitakuwa madhihirisho yake makuu.

Matini ya ujumbe wa Kiongozi Muadhamu ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Baada ya kumalizika muda wa miaka mitano wa uongozi wako katika Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ninakupongeza kwa juhudi kubwa zilizofanyika katika kuendesha taasisi hiyo kubwa na huduma ulizotoa wewe na wenzako katika nyanja mbalimbali na ninakuteuwa kuendeleza kazi hiyo nzito na nyeti kwa kipindi kingine.

Daima unapasa wewe na wakurugenzi wenzako kutilia maanani mafanikio ya sasa ya Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB) na mapungufu yake na kufanya mlinganisho baina yao. Jitihada za kuondoa nakisi katika utendaji wa chombo hicho hazipaswi kupungua au kuzembea.

Maagizo yangu muhimu ni kukikurubisha chombo hicho muhimu cha kiutamaduni katika daraja ya chombo cha habari ambacho dini, maadili mema, matumaini na kuelimisha jamii ndio sifa zake kuu. Chombo hicho kinapaswa kuwa kigezo cha mwenendo wa kijamii ya wafuatiliaji wake na taasisi muhimu kamafamilia. Vilevile sanaa na mbinu mbalimbali za kiufundi zilizojaribiwa au za kisasa zinapaswa kutumiwa barabara katika kuhudumia ustawi wa vigezo hivyo.

Kuna udhaura wa kutumia uzoefu wenye mafanikio au ukosefu wa mafanikio wa kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kukifikisha chombo hiki katika kiwango cha juu na kukamilisha au kusahihisha harakati za shirika hilo kwa kupanga ratiba ya vipindi na kuainisha vigezo.

Inatarajiwa kuwa dalili za mabadiliko hayo zitaonekana katika mwaka wa kwanza za kazi zako. Ninakutakia taufiki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Sayyid Ali Khamenei

16 Aban 1388 (07 November 2009)

700 /