Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Rambirambi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia kifo cha Ayatullah Muntadhari

Nimepokea habari ya kufariki dunia mwanachuoni na fakihi mkubwa Alhaj Sheikh Husainali Muntadhari (Mwenyezi Mungu amrehemu). Mwachuoni huyo alikuwa ni fakihi aliyetabahari na mwalimu mkubwa ambaye wanafunzi wengi wamestafidi na elimu yake. Kipindi kikubwa cha maisha yake alikipitisha katika kutumikia harakati ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amridhie) na alifanya jitihada kubwa na kuvumilia matatizo mengi katika njia hiyo.

Katika kipindi cha mwishoni mwa maisha yaliyojaa baraka ya Imam Khomeini (MA), ulitokea mtihani mzito na wa hatari na ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu na amghufirie faqihi huyu na ajaalie mitihani iliyomkumba hapa duniani iwe ni kafara kwake.

Ninatoa mkono wa pole kwa wafiwa wote hususan mke na watoto wa marehemu huyo nikimuombea rehema na maghufira ya Mwenyezi Mungu Mwingi wa kurehemu.

Sayyid Ali Khamenei

29/Azar /1388

 

700 /