Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Salamu za rambirambi za Kiongozi Muadhamu kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Dakta Ali Muhammadi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei ametoa ujumbe wa salamu za rambirambi kutokana na kuuawa shahidi Dakta Mas'ud Ali Muhammadi.

Matini kamili ya ujumbe huo ni hii ifuatayo:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehma, Mwenye kurehemu.

Ninatoa mkono wa pongezi na salamu za rambirambi kwa mama, mke, jamaa, marafiki, wanafunzi na wafanyakazi wenzake shahidi Ustadh msomi marehemu Dakta Mas'ud Ali Muhammadi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwa mnasaba wa kuuawa shahidi msomi huyo.

Mkono wa jinai uliohusika na mauaji hayo umefichua malengo ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ni kutoa pigo kwa harakati na jihadi ya kielimu hapa nchini.

Hapana shaka kuwa hima na ari ya wasomi, wahadhiri na watafiti hapa nchini itakwamisha malengo hayo.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe daraja za juu peponi shahidi huyo aliyepata ufanisi na awape subira na ujira mwema ndugu za jamaa zake.

Sayyid Ali Khamenei

25 Day 1388

15 Januari 2010   

 

700 /