Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu:

Jamii inapaswa kuanisika kwa kitabu

Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo asubuhi ametembelea Maonyesho ya 23 ya Vitabu ya Kimataifa ya Tehran. Ayatullah Khamenei amezungumza na wachapishaji na waandishi vitabu kwenye maonyesho hayo kuhusu soko la uchapishaji na vitabu vipya.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea kuridhishwa na maonyesho ya vitabu ya mwaka huu na akasema: "Kusoma vitabu ni moja ya kazi za kimsingi maishani na iwapo tutakuwa na imani hiyo basi hakuna kazi itakayozuia usomaji vitabu."

Ayatullah Khamenei amesisitiza juu ya kuzidishwa uchapichaji na usomaji vitabu nchini na akaongeza kuwa jamii inapaswa kuanisika kwa kitabu.

Ayatullah Khamenei alianza kutembelea vyumba vya Maonyesho ya 23 Vitabu ya Kimataifa ya Tehran saa tatu asubuhi akifuatana na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu na kukagua vyumba na sehemu mbalimbali za maonyesho hayo akiuliza maswali kuhusu hali ya uchapishaji na vitabu vipya.    

700 /