Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa rambirambi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia kifo cha Ayatullah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu

Kufuatia kifo cha mwanazuoni mwanajihadi Ayatullah al Haj Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah (Mwenyezi Mungu amrehemu) ninatuma rambirambi na mkono wa pole kwa familia ya Fadhlullah, marafiki na wapenzi wa marehemu nchini Lebanon, jamii za Walebanon katika mabara ya Afrika na America ya Latini na kwa mashia wote wa Lebanon. Mwanazuoni huyu mkubwa aliyekuwa na bidii alikuwa na taathira katika medani za dini na siasa, na Lebanon haitasahau huduma na baraka zake kwa miaka mingi.

Katika kipindi chote cha umri wake harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon ambayo ina haki kubwa juu ya umma wa Kiislamu, imefaidika na himaya, ushirikiano na msaada wa mwanazuoni huyo mpiganaji jihadi.

Ayatullah Fadhlullah pia alikuwa mtetezi mwenye ikhlasi na shupavu wa Jamhuri ya Kiislamu na daima alithibitisha kwa maneno na vitendo uaminifu wake kwa Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi chote cha miaka thalathini iliyopita.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ateremshe rehma na maghufira yake kwa roho ya sayidi huyo sharifu na azizi na amfufue pamoja na mababu zake watoharifu.

Sayyid Ali Khamenei

Tarehe 14 Tir 1389 (05/07/2010)

  


700 /