Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Katika ujumbe wake kwa Waislamu wote dunia kwa mnabasa wa maafa makubwa ya mafuriko nchini Pakistan, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu asema:

Tuwasaidie haraka ndugu zetu waliopatwa na masaibu wa Pakistan kwa msingi wa udugu wa Kiislamu

Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma, Mwenye kurehemu

Kwa umma adhimu wa Kiislamu

Maafa ya mafuriko yaliyowatumbukiza kaka na dada zetu Waislamu wa Pakistan katika mtihani mkubwa yanazidi kupanuka siku baada ya siku. Maafa hayo yameyakumba maeneo mengi ya kaskazini hadi kusini mwa Pakistan na kuwalazimisha mamilioni ya watu kukimbia nyumba zao. Ukubwa wa maafa hayo ya kusikitisha pia umetatiza mno kazi ya kuwafikishia misaada waathirika.

Taifa la Waislamu la Pakistan limepatwa na masaibu hayo makubwa katika hali ambayo vikosi vya jeshi vamizi la Marekani vinaendelea kushambulia vikali ardhi ya nchi hiyo ya Kiislamu kwa kutumia visingizio mbalimbali.

Enyi mataifa ya Kiislamu

Kiwango cha hasara iliyosababishwa na mafuriko hayo ni kikubwa mno kiasi kwamba mbali na mahitaji ya dharura na ya haraka ya chakula, mavazi na makazi ya ndugu zetu, sehemu kubwa ya miundombinu ya Pakistan pia imetoweka. Inasikitisha kwamba jumuiya za kimataifa hazijatekeleza ipasavyo wajibu wao yaani kuwahudumia watu waliopatwa na masaibu; jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na kuchunguzwa kwa makini.

Ndugu zangu Waislamu  

Kiwango cha misaada yetu -kadiri kitakavyokuwa- ni kidogo mno kikilinganishwa na mahijati makubwa ya watu waliokumbwa na mafuriko nchini Pakistan. Hata hivyo inatupaswa katika kipindi hiki nyeti tutekeleze wajibu wetu kwa mujibu wa udugu wa Kiislamu na kupeleka misaada haraka kwa ndugu zetu waliopatwa na masaibu.

Jambo linalopaswa kutiliwa maanani zaidi na nchi za Kiislamu na jumuiya za kimataifa ni kuisaidia serikali ya Pakistan katika kupanga na kutekeleza mipango ya kukabiliana na masaibu hayo na pia jinsi ya kuwasilisha misaada na taathira za sasa na za kipindi kirefu za maafa haya; masuala ambayo kwa hakika yanaweza kuisababishia matatizo serikali yoyote katika suala la kufikisha misaada kikamilifu na kwa pande zote kwa waathirika wakati wa dharura.

Sayyid Ali Khamenei

9 Shahrivar 1389

20 Ramadhani Tukufu 1431 (31/08/2010)


700 /