Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu azuru makaburi ya mashahidi wa Qum

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei mapema leo akiwa katika siku ya tano ya safari yake katika mji mtakatifu wa Qum ametembelea makaburi ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa mji huo na kuwasomea suratul Fatiha. Ayatullah Khamenei pia amewaombea dua na daraja za juu peponi mashahidi hao.

Baadaye Ayatullah Khamenei amezuru makaburi ya Hazrat Ali bin Ja'far.

Vilevile alizuru makaburi ya Sheikhan na kuwasomea al Fatiha maulama wakubwa kama Zakaria bin Adam, Mirza Qummi na Mirza Jawad Agha Malaki Tabrizi.

 

700 /