Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu atembelea maonyesho ya vituo vya utafiti vya Qum

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya leo ametembelea maonyesho ya athari za kielimu na uhakiki uliofanywa na zaidi ya vituo 70 na taasisi za utafiti wa Kiislamu za Qum. Ayatullah Khamenei ametumia masaa manne katika kutembelea maonyesho hayo yaliyopewa jina la Mishkat.

Taasisi na vituo vya utafiti wa masuala ya Kiislamu vimeonyesha mafanikio na bidhaa zao ikiwa ni pamoja na makala za utafiti, tasnifu za wanachuo wa daraja za uzamili na uzamivu, uhakiki unaofanywa na vyuo vya kidini na programu za komputa za sayansi na elimu za Kiislamu.

Baadhi ya athari zilizoko katika maonyesho hao zinajumuisha majibu ya maswali ya vjana kuhusu maswala ya kidini na Kiqur'ani.

Baadhi ya makala na vitabu vilivyoko katika maonyesho hayo vinahusu misingi ya kinadharia na kimatendo ya maadili ya Kiislamu, mijadala ya ufati wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu, maarifa ya Kiislamu, dua na elimu ya teolojia, makala za uchunguzi kuhusu Shia, uchunguzi wa hadithi, mjadala wa Imam Mahdi (as) na majibu ya maswali ya kiitikadi na kifikra ya vijana, sheria za fiqhi, sayansi ya Qur'ani, elimu ya nujumu, na utafiti wa Nahjul Balagha.

Vyumba vya maonyesho vya maktaba ya Ayatullah Mar'ashi Najafi, Kituo cha Utafiti na Majibu ya Maswali, taasisi za elimu za hauza na maktaba mbalimbali za Qum pia zinaonyesha mafanikio na kazi zao katika maonyesho hayo.

Programu za komputa zilizoshinda za hauza hususan maktaba ya dijitali ya vitabu vya Kiislamu pia zinaonyeshwa katika maonyesho ya Mishkat.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliswali swala ya Magharibi wakati anatembelea maonyesho hayo na baadaye akaendelea kutembelea vyumba mbalimbali.  

      

700 /