Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu akijibu barua ya wasomi vijana:

Ninaitoa zawadi hii kwa Haram ya Imam Ali bin Mussa Ridhaa (as)

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Atayullah Ali Khamenei amewashukuru wasomi 13 vijana wa Iran waliomtunuku medali zao walizoshinda katika mashindano ya kielimu na kuzitoa zawadi medali hizo kwa Haram Tukufu ya Imam Ridha (as).

Wasomi hao 13 vijana hivi karibuni walimwandikia barua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wakimtunuku medali zao 15 walizoshinda katika mashindano ya olimpiadi za kitaifa na kimataifa. Ayatullah Khamanei amejibu barua hiyo akisema:

Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehma, Mwenye kurehemu

Ninawashukuru ninyi vijana azizi ambao ni nuru ya macho ya taifa kubwa la Iran na wamulikaji wa upeo wa mustakbali wa nchi hii. Ninaitoa zawadi hii yenye thamani kwa Haram Tukufu ya Abul Hassan Ali bin Mussa Ridha, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.

Ninawatakia taufiki.

Sayyid Ali Khamenei

5 Dei 1389  (26 Disemba 2010)  

  

           

700 /