Tovuti ya Habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamenei

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu waelekea Madina kuwasilisha rambirambi

Wawakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei wameelekea katika mji mtakatifu wa Madina kuwasilisha salamu za rambirambi za Kiongozi Muadhamu kufuatia kifo cha Allamah Sheikh Muhammad Ali al Amri ambaye alikuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia. Ayatullah Ahmad Jannati na Hujjatul Islam Marvi wametumwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei kwenda mjini Madina kwa shabaha ya kuwasilisha rambirambi za kiongozi huyo kwa familia ya Ayatullah al Amri na kushiriki katika majlisi ya kumuombea rehma na maghufira mwanazuoni huyo.

700 /